Na Mwandishi Wetu, Arusha
Wajumbe kutoka nchi 12 za Afrika ambao pia ni wawakilishi kutoka Chama cha Mifuko ya Matengenezo ya Barabara Barani Afrika (ARMFA), wametembelea na kujionea maendeleo ya uwanja wa michezo Arusha.
Ziara ya kutembelea uwanja ilifanyika kwa maelekezo ya Waziri wa Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Abdallah Ulega, kwa Rais wa ARMFA ambaye ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Tanzania, Mhandisi Rashid Kalimbaga, ili kuwaonesha wageni hao maendeleo ya mradi huo wa ujenzi wa uwanja wa michezo.
Wajumbe hao waliokuwa jijini Arusha kwa ajili ya hafla rasmi ya makabidhiano ya Urais wa ARMFA, wameongeza ziara yao kwa kutembelea uwanja huo, uliowajumuisha wawakilishi wa Mifuko ya Matengenezo ya Barabara Barani Afrika, ulikutana nchini Tanzania kwa ajili ya tukio la kihistoria la mabadiliko ya uongozi ndani ya chama hicho.
Katika ziara hiyo, wajumbe walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya mradi ili kujionea ukubwa, kasi na ubora wa kazi zinazofanyika.
Pia, ziara hiyo ilionesha dhamira ya Tanzania katika kuendeleza miundombinu ya kisasa ya michezo inayokidhi viwango vya kimataifa.
Hii inakuja huku Afrika Mashariki ikiendelea na maandalizi ya kuandaa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, yatakayofanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 18, 2027, kwa ushirikiano wa Tanzania, Kenya na Uganda.
Ambapo mradi wa uwanja wa Arusha unasimama kama ishara ya ushirikiano wa kikanda, uwekezaji wa kimkakati na utayari wa kuandaa mojawapo ya matukio makubwa zaidi ya michezo barani Afrika.

No comments:
Post a Comment