WATAALAMU WA UBIA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAJADILI UBIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 5, 2026

WATAALAMU WA UBIA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAJADILI UBIA


Mchumi Mkuu kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bi. Josephina Melkiol Buhili, akifungua kikao cha Wataalamu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kutoka Wizara ya Fedha, Tanzania, Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) na Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Zanzibar, kwa niaba ya Kaimu Kamishna wa Kitengo cha PPPU, Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, ikiwa ni sehemu ya Kikao cha Kwanza Cha ushirikiano kati ya pande zote mbili kwenye masuala ya PPP, kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.kinachofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Dar Es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Wizara ya Kazi na Uwekezaji- Zanzibar, Bi. Bihindi Nassor, akizungumza wakati wa kikao cha Watalamu wa Masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha, Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Tanzania na wataalamu kutoka Idara ya ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPD), Wizara ya Kazi na Uwekezaji- Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Kikao cha Kwanza Cha Ushirikiano kati ya pande zote mbili kwenye masuala ya PPP, kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, kinachofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar Es Salaam.

Mchumi Mkuu kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bi. Josephina Melkiol Buhili, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Wizara ya Kazi na Uwekezaji- Zanzibar, Bi. Bihindi Nassor, wakati wa kikao cha Wataalamu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kutoka Wizara ya Fedha, Tanzania na Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Zanzibar, kilichofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo jijini Dar Es Salaam.

Mchumi Mkuu kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bi. Josephina Melkiol Buhili, akitoa wasilisho wakati wa kikao cha wataalamu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kutoka Wizara yaa Fedha, Tanzania na Wizara ya Kazi na Uwekezaji Zanzibar, kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar Es Salaam.

Wataalam wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), pamoja na Wataalamu kutoka Idara ya Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPD), Wizara ya Kazi na Uwekezaji- Zanzibar, wakifuatilia wasilisho la Mchumi Mkuu kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bi. Josephina Melkiol Buhili (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar Es Salaam.

Mchumi kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bi. Anastazia Amandi, akitoa wasilisho kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Misaada ya Kibajeti na Madeni Sanjari (Draft Fiscal Commitment Liability - FCCL), wakati wa Kikao cha Wataalamu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, kutoka Wizara ya Fedha, Tanzania pamoja na Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Zanzibar, kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar Es Salaam.

Afisa Mwandamizi Msimamizi wa Fedha, Idara ya Maandalizi na Uchambuzi wa Miradi kutoka Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Bi. Mwanaidi Araba, akizungumza wakati wa Kikao cha Wataalamu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, kutoka Wizara ya Fedha, Tanzania pamoja na Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Zanzibar, kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Wizara ya Kazi na Uwekezaji- Zanzibar, Bi. Bihindi Nassor (Katikati, mstari wa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Mchumi Mkuu kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bi. Josephina Melkiol Buhili (watatu kushoto), Afisa Mwandamizi Msimamizi wa Fedha, Idara ya Maandalizi na Uchambuzi wa Miradi kutoka Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Bi. Mwanaidi Araba, Mchumi kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bi. Anastazia Amandi (wa kwanza kulia) pamoja na wataalamu wengine wa masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) mara baada ya kikao cha wataalamu hao katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar Es Salaam.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar Es Salaam)


Na Asia Singano, WF, Dar Es Salaam.


Wataalamu kutoka Kitengo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), na Wataalam kutoka Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Zanzibar, kupitia Idara ya Mashirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPD), wamekutana na kujadili kuhusu maandalizi ya Kikao cha Kwanza cha Ushirikiano kati ya pande zote mbili kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar Es Salaam.

Katika kikao hicho wataalamu hao walijadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitia na kuthibitisha ajenda zitakazojadiliwa katika Kikao cha Kwanza cha Ushirikiano huo.

Wataalamu hao pia walipitia taarifa ya utekelezaji wa yatokanayo na kikao cha pili cha Ushirikiano kwa mwaka wa fedha 2024/2025, na kupata wasilisho kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Misaada ya Kibajeti na Madeni Sanjari.

No comments:

Post a Comment