
Kaimu Mkuu wa Polisi Jamii Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Mkaguzi wa Polisi (INSP) Christopher Newton amewataka Askari Mgambo kuzingatia ukamataji salama unaozingatia misingi ya haki za binadamu.
Kauli hiyo imetolewa leo Machi 31, 2026 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Ilala Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Askari hao ambao wameajiriwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali zilizoanzishwa na Halmashauri hiyo kwa mustakabali wa maendeleo ya wananchi wake.
INSP Newton amesema “Jeshi la Polisi kupitia falsafa ya Polisi Jamii imeanzisha programu ya ukamataji salama ambapo katika programu hiyo inaelekeza wananchi mmoja mmoja na vikundi vya ulinzi shirikishi tahadhari wanazopaswa kuzichukua wakati wa ukamataji ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, taratibu na masharti wakati wa ukamataji wa wahalifu. Hivyo niwatake wote kwa pamoja katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku kwenda kufuata maelekezo hayo ili kuzuia malalamiko ya uvunjifu wa haki za binadamu”.


No comments:
Post a Comment