
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na watendaji wa Polisi kutoka Kamisheni ya Ushirikishwaji wa jamii Makao Makuu ya Polisi wametoa pole kwa wanafunzi na walimu wa shule msingi Swaswa kufuatia ajali ya vifo vya wanafunzi watatu waliofariki wakati wakiogelea katika bwawa.
Akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule hiyo Aprili 29, 2026 Polisi Kata ya Ipagala Mkaguzi wa Polisi (INSP) Emmanuel Nungwana ametoa salamu za pole na kuwataka walimu, wazazi pamoja na walezi kuongeza umakini katika suala la malezi ili kuhakikisha watoto wanakua salama wakati wote nyumbani na shuleni.
Aidha, INSP Emmanuel amewataka wanafunzi kuepuka michezo hatarishi, utoro mashuleni na kuhakikisha wanafuata ratiba za shuleni na nyumbani hususani maelekezo sahihi ya walimu na wazazi.
Vilevile, watendaji kutoka Kamisheni ya Ushirikishaji wa Jamii Makao Makuu ya Polisi wamewataka wanafunzi kuwa wa wazi kwa kutoa taarifa za viashiria vyovyote vya uhalifu sambamba na kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya wanafunzi wanayotendewa nyumbani na shuleni.
Uongozi wa shule ya Msingi Swaswa na wanafunzi wamepongeza ujio wa Jeshi la Polisi na kutoa elimu itakayo saidia wanafunzi, walimu na walezi kudhibiti na kukabiliana na matukio ya uhalifu pamoja na matukio yanayoweza kuleta taharuki na simanzi kwa jamii.







No comments:
Post a Comment