KITUO KIPYA CHA UCHENJUAJI MADINI KUJENGWA MWAKITOLYO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 15, 2026

KITUO KIPYA CHA UCHENJUAJI MADINI KUJENGWA MWAKITOLYO



Na Mwandishi Wetu - Dodoma


Serikali kupitia Wizara ya Madini inatarajia kujenga Kituo kipya cha Mfano cha Uchenjuaji Madini katika eneo la Mwakitolyo mkoani Shinyanga.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 15, 2026 na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa wakati akijibu swali Bungeni lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Mwanahamisi Athuman, aliyetaka kujua kuhusu Mpango wa Serikali kuanzisha chuo cha madini Mkoani Shinyanga.

Dkt.Kiruswa amesema kuwa, Serikali inatambua umuhimu wa Mkoa wa Shinyanga katika sekta ya madini pamoja na uhitaji wa kuwajengea uwezo wananchi wake, wakiwemo vijana na wanawake katika shughuli za utafiti , uchimbaji na Uchenjuaji madini.

Dkt. Kiruswa ameeleza kuwa, kwasasa Serikali inaendelea kutumia vyuo vyake katika kufundisha taaluma za madini kupitia vyuo villivyopo katika mkoa wa Dar es salaam na Tabora.

Aidha, Dkt. Kiruswa ametoa wito kwa wananchi hususan vijana kujitokeza kunufaika na huduma na mafunzo zinazotolewa na vyuo mbalimbali vya Serikali kikiwemo Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kilichopo mkoani Arusha na Chuo Cha Madini Dodoma (MRI) ambavyo vinafundisha taaluma za madini.

No comments:

Post a Comment