
WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Serikali itaendelea kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa kutosha kukidhi mahitaji ya ndani na ziada kwa ajili ya kuuza nje ili kuongeza mapato ya fedha za kigeni.
Akiwasilidha hotuba yake bungeni jijini Dodoma, Mhe. Ndejembi amesema katika mwaka wa fedha 2026/27 wizara itaweka mkazo katika kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika mijini, vijijini na vitongojini pamoja na kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.
Amesema pia Serikali itaendelea kuwekeza katika shughuli za utafutaji, uendelezaji, uzalishaji na usambazaji wa mafuta na gesi asilia ili kuhakikisha nchi ina uhakika wa upatikanaji wa nishati hiyo muhimu kwa maendeleo ya uchumi.
Aidha, amebainisha kuwa jitihada zaidi zitaelekezwa katika ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhi na kusambaza bidhaa za mafuta ili kuongeza ufanisi na upatikanaji wake nchini.

No comments:
Post a Comment