SERIKALI YAKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, April 10, 2026

SERIKALI YAKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA


Na Mwandishi wetu


Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukingozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi,
imekutana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na Rais wa
zamani wa Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera, na kujadiliana kuhusu
namna Tanzania ilivyojidhatiti katika kudumisha umoja, amani na mshikamano
miongoni mwa Watanzania.

Kikao hicho kilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyrere (JNICC) siku ya Alhamisi Aprili 9, 2026 mchana baada ya Mheshimiwa
Chakwera kumtembelea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. Balozi Mahamoud Thabit Kombo, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa ziara ya
Mjumbe huyo Maalum nchini Tanzania.

Katika kikao hicho, Mhe. Profesa Kabudi alimueleza kwa kina Mjumbe huyo Maalum,
kuhusu hatua mbalimbali zinazoendelea kuchululiwa na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuimarisha demokrasia nchini huku ikiweka
mssisitizo katika kulinda na kuheshimu utu wa Mtanzania, kuzingatia haki na uwajibikaji,
amani na utulivu pamoja na kudumisha umoja wa kitaifa.

“Tumekutana na Mheshimiwa Chakwera na tumemueleza mambo mengi kuhusu
Tanzania na historia ya nchi hii tangu ipate uhuru mwaka 1961, hali ya siasa na
demokrasia nchni, na hatua ambazo serikali inaendelea kuchukua ili kuhakikisha nchi
inaendelea kuwa tulivu na kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika kujenga
uchumi jumuishi na kujiletea maendeleo”, ameeleza Waziri Kabudi.

Waziri kabudi ameeleza kuwa kikao hicho kimekuwa kizuri na chenye mafanikio
kutokana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kupata ufafanuzi
wa kutosha juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini hususani katika
kudumisha amani, umoja wa kitaifa na ustawi wa Watanzania.

Mbali na kukutana na ujumbe wa Serikali, Mheshimiwa Chakwera anatarajiwa kukutana
na wadau mbalimbali ambapo jana Aprili 10, 2026 alikutana na Msajili wa Vyama vya
Siasa, Mhe. Jaji Mstaafu Francis Mutungi pamoja na vyama vya siasa vya ACT–
Wazalendo, Chama cha National League for Democracy (NLD), United Democratic
Party (UDP), Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Chama cha NCCR
Mageuzi, Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Alliance for Democratic
Change (ADC), Alliance for African Farmers Party (AAFP) na Chama cha ADA-TADEA.

Vyama vingine ni pamoja na Democratic Party (DP), Tanzania Labour Party (TLP),
Union for Multiparty Democracy (UMD), United People’s Democratic Party (UPDP),
Chama cha Kijamii (CCK), Demokrasia Makini, Chama cha Ukombozi wa Umma
(CHAUMA) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika ziara yake hii, Mheshimiwa Chakwera anatarajia pia kukutana na Mwenyekiti wa
Tume ya Uchunguzi wa matukio yaliyotokea Oktoba 29, 2025 na baada ya Uchaguzi
Mkuu, Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Othman Chande, Waziri Mkuu Mstaafu na
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jaji Joseph
Warioba, Jumuiya zisizo za Kiserikali, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,
Mhe. Jaji George Joseph Kazi, Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo Mhe. Othman Masoud
Othman, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan
Zungu, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jaji
George Mcheche Masaju, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu
wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele na Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi Mhe. Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro.

Aidha, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, atakutana pia na
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
pamoja na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment