Na Mwandishi wetu Itigi, Singida
Timu kutoka Uganda ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii, Wanyamapori na Malikale Bi. Doreen S. Katusiime yafanya ziara ya mafunzo Itigi.
Timu hiyo ipo nchini Tanzania na jumanne tarehe 21, Aprili 2026 imetembelea vikundi na miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya mradi wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya nyara ( IWT Project).
Miongoni mwa vikundi vilivyotembelewa ni pamoja na Jumuiya ya wafuga nyuki Muhesi na kikundi cha Nyukimali Doroto Itigi mkoani Singida.
Huu ni mpango maalumu wa ziara za mafunzo baina ya nchi zinazotekeleza Miradi yenye malengo yanayoshabihiana ili kubailishana uzoefu na kujifunza namna nchi nyingine inavyotekeleza Mradi wake.










No comments:
Post a Comment