TCDC SPORTS CLUB YASHIRIKI MASHINDANO YA KARATA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, April 25, 2026

TCDC SPORTS CLUB YASHIRIKI MASHINDANO YA KARATA



Timu ya Wachezaji wa Karat a upande wa Kike na kiume zimeshiriki Mashindano ya mchezo wa Karata leo Aprili 25, 2026 katika viwanja vya Sabasaba mkoani Njombe.

Upande wa kike mshiriki Godlove Kyangala alichuana vikali na Timu ya Maliasili na kujinyakulia pointi nne (4) baada ya kumfunga Maliasili mzunguko yote miwili.

Mzunguko wa pili TCDC ilicheza na Wizara ya Madini na kupata pointi mbili (2) kwa mzunguko wa kwanza na mzunguko wa pili Timu zote mbili zilitoa sare ya mbilimbili.

Mzunguko wa tatu TCDC ilicheza na Uchukuzi na matokeo kuwa sare,ambapo kwa mzunguko wa nne TCDC ilipoteza pointi nne kwa kufungwa na timu ya IRDT na mzunguko wa tano na mwisho TCDC ilipoteza pointi nne dhidi Uwekezaji.

Kwa upande wa timu ya Karata ya kiume mshiriki alikuwa ni Zawadi Joseph ambapo mzunguko wa kwanza alicheza na Uchukuzi na matokeo kuwa sare ya mbili kwa mbili, mzunguko wa pili matokea pia yalikuwa sare Kati ya TCDC na Uwekezaji, mzunguko wa tatu kati ya TCDC na mzunguko wa tatu TCDC ilitoka sare tena dhidi ya TAKUKURU.

Mzunguko wa nne, TCDC ilipoteza pointi tatu dhidi ya Wizara ya Maji na kupoteza tena pointi tatu kwenye mchezo wake dhidi ya Ulinzi katika mzunguko wa tano.Katika mzunguko wa sita na wa mwisho Dodoma Jiji ilijinyakulia pointi nne kwa sifuri kwa TCDC.

Kwa matokea hayo TCDC Sports Club upande wa Karata Timu zote mbili hazikufanikiwa kuvuka hatua za makundi 16 bora katika michezo hiyo ya Meimosi.

Hapo Kesho Aprili 26, 2026, Jackson Mkoloweko na Grace Mnare wanatarajia kushiriki mchezo wa Bao utakaochezwa saa 2:30 asubuhi katka viwanja vya Sabasaba mkoani humo.

No comments:

Post a Comment