WATAALAM WA MAABARA KUTUMIA VIWANGO VYA KIMATAIFA UCHUKUAJI, UFUNGASHAJI NA USAFIRISHAJI WA SAMPULI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 28, 2026

WATAALAM WA MAABARA KUTUMIA VIWANGO VYA KIMATAIFA UCHUKUAJI, UFUNGASHAJI NA USAFIRISHAJI WA SAMPULI



Na Atley Kuni, WAF-Morogoro


Wizara ya Afya kwa kushirikiana na mdau KOFIH imewapa mafunzo ya siku tatu Wataalam wa Maabara nchini wanaotarajiwa kutumia miongozo yenye viwango va kimataifa wakati wa kukusanya, kufungasha na kusafirisha sampuli za vipimo vya kipindupindu nchini.

Hayo yameelezwa April 28, 2026 mkoani Morogoro na Mratibu wa Mafunzo hayo Bw. Emmanuel Magembe wakati wa mafunzo ya siku tatu yanayolenga kuwaimarisha wataalamu wa maabara ngazi ya wilaya.

"Ninyi ni mabalozi wetu ambao mmeteuliwa kuja hapa kutoka wilaya ambazo zinapata milipuko ya mara kwa mara ya ugonjwa wa kipindupindu, ni imani kwamba mafunzo haya yatawanoa vizuri katika eneo la ukusanyaji,upimaji , na usafirishaji wa sampuli za kipundupindu, " amesema Magembe.

Akizungumza na wataalam hao Bi. Olympia Machange Mratibu wa mradi unaowezesha mafunzo hayo kupitia Maabara ya Taifa unaofadhiliwa na Korean Foundation for International Healthcare (KOFIH), amefafanua kwamba mafunzo hayo ni mwendelezo wa kazi mbalimbali zinazofanywa katika mradi huu wa miaka mitano.

"Serikali inategemea mara baada ya mafunzo haya, muwe na uwezo wa kuwafundisha watalaam waliobakia vituoni ili tuwe na wataalamu wengi wenye uwezo wa usimamizi wa sampuli za kipindupindu ngazi ya wilaya" amesema Bi. Olympia.

Mmoja ya Watoa mada kwenye mafunzo hayo kutoka maabara ya Taifa, Bw. Modest Chuwa, amewaasa wataalam hao kuisaidia jamii, kwa kutoa elimu ya upimaji wakati wanatekeleza majukumu yao ili waweze kupata ushirikiano wa moja kwa moja kutoka kwa jamii ili kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu.





No comments:

Post a Comment