MKANDARASI ATAKIWA KUONGEZA KASI MRADI WA MAJI MAFINGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 9, 2026

MKANDARASI ATAKIWA KUONGEZA KASI MRADI WA MAJI MAFINGA



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Rose Ambrose, amemtaka mkandarasi wa Mradi wa Maji wa Miji 28 Mafinga kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili wananchi wa Mafinga na maeneo jirani waanze kupata huduma ya majisafi na salama.

Bi. Rose amesema hajaridhishwa na maendeleo ya mradi huo na kusisitiza kuwa hakuna sababu ya kuchelewesha utekelezaji wake. Amesema Serikali inahitaji kuona kazi muhimu ikiwemo ujenzi wa bwawa na miundombinu mingine ikiendelea kwa kasi.

Aidha, amemtaka mkandarasi huyo kuwasilisha Wizara ya Maji mpango kazi wa haraka utakaobainisha namna atakavyoongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo hadi kukamilika kwake kwa wakati.

Ameeleza kuwa Serikali haitakubali kuona mradi huo ukiendelea kusuasua kwani unalenga kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa Mji wa Mafinga na maeneo ya jirani.

Mradi huo unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 109,720 wa kata saba za Halmashauri ya Mji wa Mafinga na kuongeza upatikanaji wa majisafi na salama kutoka asilimia 67 hadi 89.



No comments:

Post a Comment