WIZARA YA MAJI YANG’ARA MASHINDANO YA MEI MOSI NA BONANZA LA OSHA NJOMBE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 2, 2026

WIZARA YA MAJI YANG’ARA MASHINDANO YA MEI MOSI NA BONANZA LA OSHA NJOMBE


Wizara ya Maji imeibuka na ushindi mkubwa katika mashindano ya Mei Mosi pamoja na Bonanza la OSHA yaliyoshirikisha Wizara, taasisi na mashirika ya umma, yaliyofanyika mkoani Njombe kuanzia Aprili 13, 2026 na kuhitimishwa rasmi Mei 1, 2026 na Mheshimiwa Rais.

Katika mashindano hayo, Wizara ya Maji ilionesha ubora wa hali ya juu kwa kujizolea jumla ya vikombe vitano na medali nne katika michezo mbalimbali, hatua iliyoiweka wizara hiyo miongoni mwa washindi wakubwa wa bonanza hilo.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, Wizara ya Maji ilitwaa nafasi ya kwanza katika mchezo wa kuvuta kamba kwa wanaume na wanawake, pamoja na ushindi wa nafasi ya kwanza katika mchezo wa draft kwa wanaume. Aidha, ilifanikiwa kushika nafasi ya pili katika mchezo wa bao kwa wanaume, sambamba na nafasi ya pili katika riadha mita 100 kwa wanaume wa kundi la wazee.

Mbali na vikombe hivyo, wizara hiyo pia ilijinyakulia medali nne katika mashindano ya riadha, hususan mbio za mita 100 na 200, zikionyesha ushindani mkubwa na uimara wa washiriki wake.

Ushindi huo unaakisi dhamira ya Wizara ya Maji katika kuhamasisha afya, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa watumishi wake kupitia michezo, sambamba na kuimarisha mahusiano na taasisi nyingine za umma nchini.







No comments:

Post a Comment