Serikali imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema hayo katika kikao na Menejimenti ya Sekta ya Maji jijini Dodoma.
Ameainisha kuwa mpango wa kufikisha maji katika vijiji ambavyo havijapata miundombinu umeanza na kasi iongozwe zaidi ambapo hivi sasa vijiji 400 katika mikoa mbalimbali vinajengewa miradi miongoni mwa vijiji 1,575. Kazi hiyo inafanyika kwa awamu.
Amesema yapo mambo ambayo amebaini yanahitaji suluhu ya haraka katika ukaguzi wa miradi aliyofanya, hivyo amewapa kazi wataalam wa maeneo hayo katika siku zisizozidi 30 kupata majibu ili wananchi waanze kunufaika na miradi ya maji.
Mhe. Aweso, kuhusu uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo ya miji nchini ametaka kufanyika kwa mpango wa dharura wa kuleta ahueni kwa wateja na mgao ukifanyika uwe wa uhalisia na muda wa kutosha.
Amesema maeneo korofi yote yanatambulika hivyo ni lazima kuyapa muarobaini ili kuwapa wateja wa maji unafuu wa kupata huduma hiyo.





No comments:
Post a Comment