MKURUGENZI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen
Kijo-Bisimba amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akitembelea kuacha
njia na kupinduka jijini Dar es Salaam.
Gari hiyo yenye namba za usajili T336 CTT aina ya Toyota LandCruiser GX
V8, lilipinduka jana asubuhi, baada ya kuacha njia katika Narabara ya
Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es Salaam.
Gari hilo lililokuwa likiendeshwa na dereva wa mkurugenzi huyo,
lilipinduka kwenye eneo maarufu la taa za Aga Khan likiwa na abiria
watatu, akiwemo Bisimba.
Akizungumza katika mahojiano na Radio One jana, Mkurugenzi Msaidizi wa
LHRC, Imelda Urio alisema Bisimba amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan
wakati abiria wengine waliruhusiwa baada ya matibabu.
No comments:
Post a Comment