Baada ya FC Barcelona kufanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0 dhidi ya klabu ya Villarreal bila kuwa na yota wao Lionel Messi ambaye bado yupo majeruhi, walipata ushindi huo katika uwanja wao wa nyumbani Nou Camp, wakati watani wao wa jadi kutoka jiji la Madrid klabu ya Real Madrid ilicheza mechi dhidi ya Sevilla katika uwanja wa Ramón Sánchez Pizjuán usiku wa November 8.
Real Marid waliingia uwanjani na staa wao Cristiano Ronaldo akiwa na rekodi yake ya nguvu ya kuifunga Sevilla jumla ya magoli 19 katika michezo 1o na kuwa na rekodi ya kuifunga Sevilla mara nyingi zaidi, rekodi ya Ronaldo haikuwa na faida katika mchezo huo kwani alishuhudia timu yake ikipokea kipigo cha jumla ya goli 3-2.
Klabu ya Real Madrid ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa beki wake Sergio Ramos dakika ya 22, goli ambalo lilidumu kwa dakika 14 pekee na Sevilla wakasawazisha kupitia kwa Ciro Immobile dakika ya 36, Real Madrid walirudi kipindi cha pili wakiwa na jitihada za kutaka kupata magoli zaidi, walijikuta wakifungwa magoli mengine mawili na Ever Banega dakika ya 61 na Fernando Llorente dakika ya 74.
Kabla ya dakika 90 hazijamalizika Real Madrid walifanikiwa kupata goli la pili kupitia kwa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia James Rodriguez dakika ya 90 ya mchezo. Kwa matokeo hayo Real Madrid watakuwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Hispania nyuma ya wapinzani wao wa jadi FC Barcelona kwa tofauti ya point tatu.
No comments:
Post a Comment