Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini ssp Advera Bulimba, amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa, maombi yote ya kufanya mikutano na maandamano yaliyotolewa na vyama vya siasa vya CCM na Chadema yamezuiliwa mpaka hapo hali itakapotengamaa baadae.
chanzo. Chanel 10
NIONAVYO:Hii inamaanisha nini kuhusu kampeni za uchaguzi mdogo,kuwa kampeni hazitatumia mikutano ya kisiasa?
Hao watu wenye mihemko wapo kiasi gani? Na kwa nini wanamihemko? Kwa sababu wameshinda au kushindwa au kudhulumiwa?
Ningeshauri polisi wetu waendeleze weledi waliouonesha kwenye kulinda mikutano ya kampeni kwa kuwaruhusu watu waandamane au hata kufanya mikutano ili kuwaondolea msongo na kuanza maisha mapya kwa #HapaKaziTu.
No comments:
Post a Comment