Jokate wa Ali Kiba Anasa Ujauzito! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 7, 2015

Jokate wa Ali Kiba Anasa Ujauzito!


Wakati Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu akihaha kuhakikisha anaitwa mama, habari ‘exclusive’ iliyotua kwenye meza ya gazeti hili inadai kuwa, mwanamitindo anayefanya pia muziki na filamu, Jokate Mwegelo amenasa ujauzito huku muhusika mkuu wa mzigo huo akidaiwa kuwa ni mpenzi wake wa sasa, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba’.

Habari hizo njema zimekuja ikiwa zimepita siku chache tangu kuwepo na taarifa kuwa mwanadada huyo yuko katika harakati za kumzalia fasta Kiba ili kukata ngebe za waliokuwa wakimsema vibaya.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, mmoja wa watu wa karibu wa Kiba aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini alisema, siku za hivi karibuni Jokate amekuwa na kila dalili za kuwa mjamzito kwani maembe mabichi kwa sana na tumbo limekuwa likimsumbua.

“Hilo la mimba ndilo linaloonekana kumsumbua kutokana na uumwaji wake na inasemekana ina miezi miwili, so kama mnaweza kufuatilia zaidi, fanyeni hivyo,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya mtoa habari huyo kunena hayo, mmoja wa waandishi wetu aliyehudhuria ‘bethidei’ pati ya Wema iliyofanyika juzi ndani ya Ukumbi wa Wema Sepetu kwenye Jengo la Millennium Towers, Kijitonyama jijini Dar alisema, akiwa eneo hilo alipata tetesi za Jokate kuwa na mimba na kwamba ndicho kilichomfanya ashindwe kutinga.

“Hizi habari za kwamba Jokate ni mjamzito nimezisikia kwenye bethidei ya Wema, imedaiwa alialikwa lakini kutokana na hali hiyo hakufika, kwa hiyo inaonekana zina ukweli,” alishadadia mwandishi wetu.

Ijumaa lamsaka Jokate
Jitihada za kumsaka Jokate kupitia simu yake ya mkononi zilifanyika ambapo awali alitumiwa sms na majibizano yakawa hivi:
Ijumaa: Mambo vipi shosti?
Jokate: Poa wangu, mzima?
Ijumaa: Salama, nasikia unaumwa, ni kweli?
Jokate: Nani amekuambia?

Ijumaa: Kuna mtu ameniambia unaumwa.
Jokate: Yeah, ni kweli.
Ijumaa: Lakini nasikia ni ugonjwa wa heri, hili likoje?
Jokate: (hakujibu).

Baada ya kupita saa kadhaa bila Jokate kujibu sms hiyo, mwandishi alianza kukata tamaa lakini juzi Jumanne usiku alimtafuta tena mwanadada huyo kwa kumpigia simu na kutoa ufafanuzi ulioshabihiana na kilichokuwa kikisemwa.
“Jamani na hilo nalo limewafikia, haya bwana ila kiukweli mimi siyo msemaji wa hayo mambo kwani ni jambo linalohusisha watu wawili,” alisema Jokate kisha akakata simu.

Kufuatia habari hizo, mashabiki wa mastaa hao kwanza wamempongeza Kiba huku wengine wakisema kuwa, kama kweli yeye ndiye kafanya kweli, basi ni kidume.
Pia wakamshauri Jokate kuamua kuzaa kutokana na umri kumruhusu, anajimudu na itamjengea heshima ya kuwa mwanamke.

Chanzo: GPL

No comments:

Post a Comment