Kauli ya Uongozi wa Diamond Baada ya Ali Kiba Kudai Diamond Ametumia Fedha Kupata Tuzo za Afrima - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 18, 2015

Kauli ya Uongozi wa Diamond Baada ya Ali Kiba Kudai Diamond Ametumia Fedha Kupata Tuzo za Afrima


Baada ya Alikiba kupost ujumbe katika Instagram akidai kuwepo na mambo yanayoendelea nyuma ya pazia kwenye muziki wake na wengi kutafsiri amelalamikia kukosa tuzo za Afrima, uongozi wa Diamond aliyeshinda tuzo tatu umezungumza.Akizungumza katika pindi cha XXL cha Clouds FM, mmoja kati ya mameneja wa Diamond, Babu Tale alisema walisikitishwa na ujumbe huo.“Mimi naona asiyekubali kushindwa sio mshindani,” alisema. “Hata sisi tumeshawahi kuingia kwenye tuzo ambazo na yeye aliongea maneno hayo alikuwepo na akashinda na hakuna mtu yeyote aliongea sijui mmenunua tuzo. Mimi nilijua mashabiki ndio wanaongea mpaka msanii anapost kitu kama kile nikahisi labda kuna mtu amehack akaunti yake. Kwahiyo nilivyoona vile nikamhukumu sio mshindani,” alisema Tale.

Hata hivyo Tale alisema baada ya kufuta kauli hiyo na kuzungumzia kauli hiyo aligundua huenda alishinikizwa na mashabiki wake.

Lakini baadaye baada ya kuona ameongea vizuri, nikagundua sometimes mtu anaweza kupaniki kwa ajili ya mashabiki wanaoongea. Lakini mwisho wa siku tunatakiwa tukae meza moja ili tusukume muziki wetu wa Tanzania. Tukiangalia line up ya muziki wa Afrika sasa hivi tupo namba mbili, tunakwenda kwenye namba 1,” aliongeza.

Hata huvyo Alikiba aliifuta post hiyo na kudai kuwa hakuandika kwa sababu alikosa tuzo.


No comments:

Post a Comment