Siku ya msanii ni siku maalum ambayo Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA)
lilibuni siku hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2008 katika kutekeleza
sheria No:23 ya mwaka 1984 iliyounda Baraza hilo. Kwa mwaka 2015
maadhimisho ya siku hiyo yalichelewa kidogo kutokana na kupisha uchaguzi
mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani.
Usiku wa December 12 zilifanyika sherehe
za maadhimisho ya siku ya msaani na kutoa tuzo nne za heshima.
Waliofanikiwa kupewa tuzo ya heshima ni Bakari Mbelemba maarufu kama mzee Jangala amepewa tuzo ya heshima ya sanaa za maonesho, Robert Yakobo amepewa tuzo ya heshima ya sanaa ya ufundi, Tekla Mjata amepewa tuzo ya heshima ya filamu na Shakira H. Said amepewa tuzo ya heshima ya sanaa ya muziki.
No comments:
Post a Comment