Matokeo:
Jumapili Mei 1
Swansea 3 Liverpool 1
Man United 1 Leicester 1
Southampton 4 Man City 2
+++++++++++++++++++
VINARA wa BPL, Ligi Kuu England, Leicester City, Leo wamesogea na kuhitaji Pointi 2 tu ili kutwaa Ubingwa baada ya kutoka Sare 1-1 na Manchester United huko Old Trafford lakini wanaweza kutwaa Ubingwa huo Kesho Jumatatu Usiku ikiwa Tottenham watashindwa kuifunga Chelsea huko Stamford Bridge.
Hii Leo Leicester walijikuta wako Bao 1 nyuma baada ya Dakika 8 tu pale Anthony Martial alipomalizia krosi ya Antonio Valencia.
Lakini
Dakika 9 baadae Kepteni wao Wes Morgan alisawazisha kwa Bao la Kichwa
alipounganisha Frikiki ya Danny Drinkwater ambae katika Dakika ya 86
alitolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya kupewa Kadi za Njano mbili.
Mapema
hii Leo, Swansea City iliichapa Liverpool 3-1 kwa Bao za Andre Ayew,
Bao 2, na moja la Jack Cork na Bao la Liverpool kufungwa na Christian
Benteke.
Dakika ya 76. Liverpool walibaki Mtu 10 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Brad Smith baada ya Kadi za Njano mbili.
Nao
Man City, wakicheza Ugenini huko Saint Mary Stadium, walichapwa Bao 4-2
kna Southampton ambao walifunga kwa Hetitriki ya Saido Mane na Bao la
Shane Long huku City wakipata Bao zao kupitia Kelechi Iheanacho.
LIGI KUU ENGLANDRatiba
**Saa za Bongo
Jumatatu Mei 2
2200 Chelsea v Tottenham
Jumamosi Mei 7
1445 Norwich v Man United
[Saa 11 Jioni]
Aston Villa v Newcastle
Bournemouth v West Brom
Crystal Palace v Stoke
Sunderland v Chelsea
West Ham v Swansea
1930 Leicester v Everton
Jumapili Mei 8
1530 Tottenham v Southampton
[Saa 12 Jioni]
Liverpool v Watford
Man City v Arsenal
Jumanne Mei 10
2145 West Ham v Man United
Jumatano Mei 11
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Norwich v Watford
Sunderland v Everton
2200 Liverpool v Chelsea
Jumapili Mei 15
**Mechi za Mwisho za Ligi, zote kuanza Saa 11 Jioni
Arsenal v Aston Villa
Chelsea v Leicester
Everton v Norwich
Man United v Bournemouth
Newcastle v Tottenham
Southampton v Crystal Palace
Stoke v West Ham
Swansea v Man City
Watford v Sunderland
West Brom v Liverpool
No comments:
Post a Comment