Wito
umetolewa kwa watu wenye ulemavu nchini kuyageuza matatizo yao kuwa fursa
baadala ya kutegemea kuonewa huruma na wahisani hali inayowafanya kudharaulika.
Hayo
yameelezwa hivi karibuni na Katibu wa chama cha wenye ulemavu mkoa wa Dodoma
Justus Ng’wantalima alipotembelewa na gazeti hili ofisini kwake kwa lengo la
kutaka kujua wamejipanga vipi kuhusiana na fursa ya ujio wa makao makuu.
Hata hivyo
katibu huyo anasema kuwa mbali na kwamba wadau mbalimbali wanajitikeza kutoa
fursa kwa watu wenye ulemavu ,hali bado si nzuri kwa jamii hii kutokana na
baadhi yao kutokuwa na utayari wa kujitoa kufanya kazi .
Amesema,ujio
wa makao makuu ni fursa kwao kwa kuwa
mahitaji yataongezeka na hivyo kuwataka watu wenye ulemavu kuchangamkia
fursa huku wakimwomba Mwenyezi Mungu kuwapa nguvu ya kutokubali kukatishwa
tama.
“Unajua,sisi
sawa ni walemavu..Lakini naamini ulemavu haumaanishi kujibweteka.Unaweza kuwa
mlemavu lakini kuna shughuli unazoweza kuzifanya zikakuingizia kipato na
ukaisaidia familia,”anasema Ng’wantalima.
Mbali na
hayo anasisitiza kuwa Mwenyezi Mungu
hakumuumba mlemavu ateseke na kujisikia mtumwa ambapo anatumia nafasi hii
kuiomba jamii kutowanyanyapaa walemavu bali wawape maarifa pale inapobidi na
kusema kuwa binadamu wote ni ndugu wanapaswa kuwa wamoja wakati wote.
Hatua hii
inatokana na kwamba baadhi ya wanajamii
wanawadharau watu wenye ulemavu na kuona kuwa hawafai kwa chochote hali
inayopelekea walemmavu kujiweka nyuma hata katika shughuli za kibiashara.
Wakati huo
huo Wanachama wa chama hicho cha ulemavu wameiomba serikali kuzingatia ujenzi
wa miundombinu na kusema kuwa iendane na mahitaji yao ili kuwarahisishia wakati wa kutafuta huduma
za kijamii.
“Mkoa wa
Dodoma umepewa hadhi ya makao makuu na hivyo majengo yanayojengwa inapaswa
yazingatie watu wenye mahitaji maalumu ”,anasema
mmoja wa walemavu .
Ili
kujikwamua kiuchumi watu wenye ulemavu mkoani hapa hufanya shughuli mbalimbali
kutokana na aina ya ulemavu ambapo wengine ni mafundi wa nguo,washona
viatu,wapaka rangi nk.
No comments:
Post a Comment