
Wakati mchezo wa Chelsea vs Manchester United ukiendelea mchambuzi mmoja wa kituo cha Sky Sports Jamie Caragher alisikika akisema Eden Hazard alikuwa bora kiasi cha kumfanya namba 10 wa timu pinzani asieleweke nini anafanya.
Caragher alimlenga Henrikh Mkhitaryan ambae wakati wote wa mchezo dhidi ya Chelsea alionekana kama mzurulaji uwanjani kwani alikuwa akitembea tu huku na huku na kazi aliyokuwa akifanya uwanjani haikujulikana.
Lakini wakati takwimu hizo zikitoka inaonesha pia kwamba Mkhitaryan dakika zake 63 aligusa mpira mara 28 tu, akidrible mpira mara moja lakini akiwa hajatengeneza nafasi hata moja wala kupiga shuti golini.
Tatizo kubwa kwa Mkhitaryan inaonekana ana tatizo linaloendana na la Romelu Lukaku kwani katika michezo yote mikubwa ambayo United wamecheza Mkhitaryan ameonekana kupwaya sana.
Kiujumla Henrikh Mkhitaryan katika michezo ambayo United wamecheza na timu zilizoko top 6 Mualmernia huyo amecheza dakika 795 na katika dakika hizo Mualmernia huyo amegusa mpira mara 614.
Tofauti na alivyokuwa Dortmund na tofauti na namba 10 wenzake Mkhitaryan anaonekana pamoja na kasi aliyonayo lakini anashindwa kufika kwa muda mipira inapofika na ndio maana hata nafasi kwa mshambuliaji wa mwisho anashindwa kutengeneza.
Msimu huu Mkhitaryan ana assists tano ambazo zimepatikana katika mechi tatu za mwanzo za Manchester United huku mechi mechi mbili kati ya hizo zikiwa dhidi ya klabu ambazo ziko tatu ya mwisho wa msimamo Epl.
Inaonekana ni muda sasa kwa Mourinho kumpa nafasi Juan Mata na kumuamini kwani wakati United wakiwaza jinsi ya kuwazuia namba 10 wa timu pinzani kubwa, wenzao hawana uwoga hata kidogo na namba 10 wa United.
No comments:
Post a Comment