Antonio Conte anaweza kutoka salama katika machinjio ya Klopp? - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 25, 2017

Antonio Conte anaweza kutoka salama katika machinjio ya Klopp?


Kwa mara ya 55 tangia karne hii iingie, hii leo vilabu vya Chelsea na Liverpool kwa mara nyingine wanakwenda kutoana jasho katika uwanja wa Anfield.

Katika michezo mitano ambayo Liverpool wamekutana na Chelsea hawajawahi kupoteza mchezo hata mmoja, Liverpool wanaonekana imara mbele ya Chelsea kwani katika mechi hizo wamepata ushindi mara mbili OT.

Lakini tangu Chelsea wapoteze mchezo zidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield mwaka 2012 hawakuwahi kupoteza mchezo mwingine zidi ya Liverpool katika uwanja huo huku wakifanikiwa kushinda mara 2 na suluhu 3.

Hadi sasa Liverpool hawajawahi kupoteza mchezo hata mmoja katika uwanja wa Anfield tangu kuanza kwa msimu huu na michezo yao 33 iliyopita katika dimba hilo wamepoteza michezo miwili tu.

Pamoja na kusemwa kuwa beki yao inapwaya sana siku za karibuni lakini Liverpool wameruhusu bao moja katika uwanja wao wa nyumbani ambapo bao hilo walifungwa wakati wakicheza na Burnley.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ana rekodi nzuri zidi ya timu zilizomaliza nafasi 6 za juu msimu
uliopita kwani tangu ajiunge na Liverpool mwaka 2015 amefanikiwa kukusanya alama 37 katika mechi 22

Lakini Antonio Conte hana rekodi mbaya sana za ugenini kwani katika michezo 12 ya ugenini msimu huu amefanikiwa kushinda michezo 10 huku akipoteza michezo miwili tu zidi ya Man City na Burnley.

No comments:

Post a Comment