Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amemtaka Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mrisho Gambo kutojaribu kufanya hila zozote za kuisababishia
CCM ipate ushindi kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika hapo
kesho, Novemba 26.
Lema amesema kwamba anafahamu kila hatua na vikao ambavyo Mkuu huyo wa Mkoa na kwamba ana ushahidi wa kutosha wa kila kitu kinachopangwa.
“Mrisho Gambo, unapaswa kujua kwamba huna mamlaka wala uwezo wa kushinda huu uchaguzi kwa nguvu/hila, hakuna kikao umekaa ambacho sina taarifa zake na ushahidi wa kila kitu” amesema Lema.
Hata hivyo, Lema ameongeza kwa kumkanya kiongozi huyo asijaribu kufanya hivyo.
“Unataka kushinda uchaguzi huu kwa gharama yoyete ile? sababu polisi wako nyuma yako? usijaribu” Lema ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter asubuhi ya leo.
Kesho Novemba 26, mwaka huu kata 43 zinatarajiwa kufanya uchaguzi wa marudio wa kuwapata madiwani.
No comments:
Post a Comment