WATHIBITI UBORA WA SHULE WAASWA KUSIMAMIA KWA WELEDI MATUMIZI YA NEST - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 12, 2026

WATHIBITI UBORA WA SHULE WAASWA KUSIMAMIA KWA WELEDI MATUMIZI YA NEST


Wathibiti Ubora wa Shule nchini wametakiwa kusimamia kwa weledi matumizi ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) ili kuhakikisha manunuzi yote ya Serikali yanafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

Rai hiyo imetolewa Juni 11, 2026 jijini Arusha na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Fredrick Salukele, akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, katika ufunguzi wa mafunzo kuhusu matumizi ya Mfumo huo.

Dkt. Salukele amesema mafunzo hayo yatawawezesha washiriki kutumia mfumo huo kwa ufanisi katika usimamizi wa fedha za uchangiaji, ununuzi wa bidhaa na huduma mbalimbali pamoja na malipo ya shughuli za tathmini za shule.

Amewasisitiza washiriki kusimamia kwa ufanisi rasilimali zilizopo, ikiwemo rasilimali watu na miundombinu, sambamba na kuimarisha huduma bora za elimu.

Aidha, Dkt. Salukele amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri na Wathibiti Ubora wa Shule kuhakikisha taasisi za elimu zinazingatia taratibu zote za uendeshaji ikiwemo masuala ya malazi, chakula na usalama wa wanafunzi.

Naye, Miurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule kutoka Wizara hiyo Dkt. Ephrahim Simbeye amesisitiza uzingatiaji wa miongozo ya elimu, akitaka kukomeshwa kwa adhabu zisizokubalika na kuhakikisha kuna mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi.

Wakizungumza kuhusu mafunzo hayo, Bi. Lilian Kasenga Mthibiti Ubora kutoka Manispaa ya Temeke pamoja na Emmanuel Hangaya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, wametaja mbinu wanazotumia kufikia malengo huku wakisema mafunzo hayo yatakwenda kuwaongezea ufanisi kazini.









No comments:

Post a Comment