Timu ya taifa ya Ubelgiji ilikuwa uwanjani usiku wa jana
kukabiliana na timu ya taifa ya Mexico ambapo katika mchezo huo Romelu
Lukaku alifunga mabao mawili kati ya matatu katika suluhu ya tatu tatu.
Eden
Hazard alifunga lingine huku mabao ya Mexico yakipatikana kupitia kwa
Andres Guardado aliyefunga kwa penati kabla ya Hirving Lozano kuongeza
mengine mawili.
Ufaransa wenyewe walikuwa uwanjani na timu yao inayosadikiwa kuwa ni kizazi cha dhahabu na kuwafunga Wales 2 kwa nunge kupitia kwa Antoine Griezman na Olivier Guroud.
Timu
ya taifa ya Ureno nao bila Cr7 walicheza na Saudi Arabia ambapo Ureno
waliibuka kidedea kwa mabao 3 kwa nunge mabao ya Ureno yakifungwa na
Fernandes, Guedes pamoja na lile la Mario.
Katika
hatua ya mtoano kuelekea kombe la dunia timu ya taifa ya Sweden
iliishtua Italia baada ya kuwafunga bao 1 kwa nunge na hivyo kuwaweka
Italia mashakani kulekea kombe la dunia 2018.
Ufaransa wenyewe walikuwa uwanjani na timu yao inayosadikiwa kuwa ni kizazi cha dhahabu na kuwafunga Wales 2 kwa nunge kupitia kwa Antoine Griezman na Olivier Guroud.
No comments:
Post a Comment