Akitoa hutoba katika bunge la Korea Kusini Trump amesema kuwa kama Korea Kaskazini inaona uvumilivu kuwa ni udhaifu inatakiwa kutambua kwamba sasa kuna utawala mpya nchini Marekani.

”Usitudharau, Usitujaribu, silaha unazozitengeneza hazikufanyi wewe kuwa salama lakini zinakuweka katika hali ya hatari” alisema Trump huku akimzungumzia moja kwa moja Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong un.

 Trump yuko katika ziara ya siku mbili nchini Korea Kusini katika ziara ya bara Asia na ameutaka ulimwengu hususani China na Urusi kuiwekea shinikizo kali Korea Kaskazini kusitisha utengenezaji wake wa silaha za kinyuklia.

                             Rais Donald Trump na Ris wa Korea Kusini Moon Jae-in

Rais huyo wa Marekani aliongeza kuwa dunia haiwezi kuvumilia hatari inayosababishwa na taifa linaloongozwa na utawala usioaminika ambao unaitishia na silaha za kinyuklia.