NI MAKUSUDI TU DEREVA ALIYEHITIMU MAFUNZO KUVUNJA SHERIA BARABARANI!!!!!! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 20, 2017

NI MAKUSUDI TU DEREVA ALIYEHITIMU MAFUNZO KUVUNJA SHERIA BARABARANI!!!!!!


Waendesha pikipiki maarufa kama Bodaboda Mkoani Dodoma wametakiwa kuyatendea kazi mafunzo wanayoyapata juu ya usalama barabarani ili kuunga mkono serikali katika kupunguza ajali za barabarani.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa chuo cha WIDE INSTITUTE OF DRIVING chenye makao yake makuu mkoani Kilimanjaro  ambayr ndiye Mkufunzi mkuu wa mafunzo hayo Ndugu FAUSTIN MATINA  wakati akifunga mafunzo hayo yaliyodumu takaribani wiki mbili katika kata ya SONGOLO wilayani CHEMBA yenye lengo la kuwafanya madereva pikipiki kujua haki zao na kuepuka uvunjifu wa Sheria za barabarani bila kujua.

Pia ameelezea masikitiko yake kwa baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo kuendelea kutenda makosa barabarani hata baada ya kupata elimu pamoja na leseni ambazo hutolewa kwa ushirikiano mkubwa ulipo kati yao na TRA  pamoja na Jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani kudai kuwa hayo ni makusudi.

“Inasikitisha sana kuona madereva waliohitimu mafunzo wanaendelea kufanya makosa barabarani  hivyo kwa nyie mnaohitimu leo nawaomba mkayazingatie haya ili kuepukana na ajali zinazozuilika” alisema Faistin Matina

Kwa upande wake Afisa huduma na elimu kwa mlipa kodi mkoa wa Dodoma Barnabas John Masika amewapongeza waliohitimu mafunzo hayo kwa muitikio wao katika kupata elimu hiyo ya usalama Barabarani na kusema mbali na kupata elimu hiyo watakuwa walipa kodi na kuliongezea mapato taifa.

Pamoja na hayo wahitimu hao wametakiwa kuweka akiba ili kuweza kuondokana na umasikini pamoja na kujiingiza katika fursa nyingine ili kuweza kujipatia pesa zaidi kwa sababu hshima ya kwanza duniani ni pesa.

"Kama huna pesa ndugu yangu hakuna lolote heshima hakuna kwa hivyo jaribu kuhakikisha unaweka akiba na mjitahidi kujiingiza kwenye biashara pia ili muweze kuongeza kipato chenu"Aliongeza Faustin Matina

Wakizungumza kwa niaba ya wahitimu wote ALLY RASHID MWAHU kutoka kituo cha Kondoa Mjini amesema mafunzo haya lazima yazingatiwe wakati AMMY ADULLAH ISUMBULA kutoka kituo cha Chemba yeye kwa upande wake amesema kuwa atawahamasisha wale ambao hawajitokeza katika kupata mafunzo hayo ili nao wajitokeze katika kipindi kingine.

Pamoja na hayo wametoa ushauri kwa Mkuu wa chuo cha WID INSTITUTE OF DRIVING  kuwa wajitahidi kuja katika kipindi ambacho wakulima wamkwishavuna mazao ya ili kutoa fursa kwa watu wngi kushiriki katika mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yanaendelea katika wilaya ya CHEMBA pamoja na KONDOA katika kata mbalimbali na lengo kubwa ni kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano katika kampeni ya kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua ama kumalizika kabisa.

HABARI PICHA;

Maandamano ya waendesha pikipiki kutoka Goima  hadi SONGOLO Wilayani CHEMBA (Picha na Okuly Julius)

Wahitimu katika kituo cha KONDOA MJINI Wakiwa na wakufunzi wao katika picha pamoja baada ya kufungwa kwa mafunzo.(Picha na Okuly Julius}

Wahitimu wakiwakatika picha ya pamoja na wakufunzi wao baada yakufungwa kwa mafunzo katika kituo cha KONDOA MJINI .(Picha na Okuly Julius)

Dereva Bodaboda kutovaa kofia  ngumu (HELEMENT) ni makusudi tuu.

wanafunzi katika kitua cha SONGOLO  wilayani  Chemba(Picha na Okuly Julius)


No comments:

Post a Comment