BARCLONA YAIWEKA REAL MADRID PABAYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 15, 2018

BARCLONA YAIWEKA REAL MADRID PABAYA

Tofauti kati ya Real Madrid na timu inayoongoza ligi (Barcelona) ni alama 19 tu lakini tofauti kati ya Real Madrid na timu nafasi ya 18  katika ligi (Deportivo La Coruna) ni alama 16 tu zikiwa ni alama 3 tofauti.

Hii inamaanisha nini? Hii inamaanisha Deportivo La Coruna wana urahisi kuifikia Real Madrid na kuwavuta hadi nafasi ya 18 ambayo ukimaliza hapo unashuka daraja kuliko Real Madrid kuwafikia Barcelona kutokana na tofauti ya alama kati ya timu hizo.

Hii imekuja baada ya kocha wa Barcelona Ernesto Valverde hapo jana kufanikiwa kupata ushindi katika uwanja wa Real Socieadad uwanja ambao makocha Pep Gurdiola, Tata Martino,Tito Vilanova na Luis Enrique walishindwa kupata matokeo.

Barcelona wakiwa kwenye moto wao walitoka nyuma kwa bao mbili na kuumaliza mchezo huo kwa ushindi wa mabao 4 huku Lioneil Messi akiweka rekodi kuwa mchezaji wa kwanza mwenye mabao mengi katika ligi moja (366).

Sasa Real Madrid wenyewe ambao ndio wapinzani wakubwa wa Barcelona kilichobaki kwao kwa sasa ni vita ya kuitetea nafasi ya 4 kwani alama zao 32 zinawafanya watofautiane na Villareal walioko nafasi ya 4 kwa alama 1 na pia watofautiane na Sevilla kwa alama 3.

No comments:

Post a Comment