
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
amesema kuwa na kibonyezo cha silaha za nyuklia kwenye meza yake wakati
wote na hivyo Marekani isithubutu kuanza vita.
Katika hotuba ya mwaka mpya
iliyopeperushwa kwa njia ya runinga, alisema kuwa Marekani inaweza
kufikiwa na silaha za nyuklia za Korea Kaskania akiongeza kuwa huo ni
kweli na wala sio vitisho.
Lakini pia alitoa wito kwa Korea Kusini kuja kwenye mazungumzo.
Korea Kaskazini pia itatuma kikosi katika mashindano ya olimpiki ya msikmu wa baridi nchini Korea Kusini, Kim alisema.
Wakati aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu vitisho vya Kim, Rais wa Marekani alisema, "tutaona, tutaona".
Alikuwa akizungumza kando mwa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya katika eneo lake ya kifahari la Mar-a-Lago huko Florida.
Korea Kaskazini imewekewa vikwazo zaidi
mwaka uliopita kwa kutokana na mipango yake ya silaha za nyuklia na
majaribio ya mara kwa mara ya silaha hizo.
Taifa hilo lililotemgwa lilifanya majaribio 6 ya nyuklia ya chini ya ardhi na kuonyesha kuongeza uwo wake wa makombora

No comments:
Post a Comment