Baada ya utawala wa Jorge Mendes katika biashara ya uwakala kuwa juu
alikuja bwana Mino Raiola raia wa Italia na wawili hawa wanatajwa kama
wafalme wa kupiga pesa katika dili za wachezaji.
Wakati Paul Pogba akipelekwa Manchester United inasemekana kwamba Raiola alipata zaidi ya 30% ya pesa alizonunuliwa Paul Pogba jambo ambalo liliishtua FIFA na kuanza kuchunguza usajili huo lakini Raiola hakukutwa na kosa.
Sasa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limeibuka na taarifa inayoonesha kiasi cha pesa ambacho mawakala wa wachezaji wamekipata katika kipindi hiki cha miaka 5 katika bara la Ulaya pekee.
Wamekula £2.3billion fedha ambayo ni asilimia 13 ya pesa ya usajili wote uliofanywa kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka huu 2017, tangu 2013 hadi mwaka jana inaonekana Ulaya kumefanyika usajili wa £19billion.
UEFA wanasema katika dili 2000 za usajili ikiwemo pia uuzaji wa timu mawakala wamepata kiasi cha £1billion pesa ambayo wanaipata kwa kuwamiliki wachezaji lakini pia kutokana na wanavyokwenda kufanya makubaliano ya kumuuza.
UEFA wametoa mfano kwa mwaka jana tu ambapo kulifanyika dili za usajili 96 katika dirisha kubwa la usajili na katika sajili zilizofanyika kuna dili 6 ambazo zote zilikuwa za mtu mmoja Jorge Mendes.
Taarifa hii ya UEFA imeshaanza kutajwa kuanza kuwavutia wafanyabiashara wengi kujiingiza katika biashara ya uwakala ambayo inaonekana kama sio ngumu sana lakini inayowaingizia pesa nyingi watu hao.

No comments:
Post a Comment