JAMAA AISHTAKI HOSPITALI BAADA YA KUSHONWA KIHUNI NA NESI 'EX WAKE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 16, 2021

JAMAA AISHTAKI HOSPITALI BAADA YA KUSHONWA KIHUNI NA NESI 'EX WAKE



KIJANA Evans Mutugi ameishitaki Hospitali ya Maura nchini Kenya kwa kitendo cha yeye kufanyia ushonaji usio kuwa wa kibinadamu na nesi ambae anadaiwa kuwa aliwahi kuwa mchumba wake (ex-girlfriend).


Tukio hilo la kustaajabisha lilitokea Jumatatu iliyopita, Novemba 8, 2021 baada ya Mutugi kupelekwa hospitalini hapo kwa matibabu ya dharura baada ya kupata ajali ya pikipiki siku ya Jumamosi, Novemba 6, 2021 majira ya mchana ambapo alipokelewa na kuhudumiwa na nesi huyo aitwaye Rose Kagwira (ex-wake).


Mutugi kupitia wanasheria wake wa John & K company ameishitaki hospitali hiyo na kudai fidia ya kiasi cha Ksh milioni 6.4 sawa na Tsh milioni 131.66


No comments:

Post a Comment