Waziri Dkt.Doroth Gwajima awapongeza Bodi,Uongozi na wafanyakazi wa Hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa ,,, - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 13, 2021

Waziri Dkt.Doroth Gwajima awapongeza Bodi,Uongozi na wafanyakazi wa Hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa ,,,



Waziri wa Afya maendeleo ya jinsia ,wazee na watoto Dkt.Doroth Gwajima (wa nne kutoka kulia) wakati wa sherehe za uzinduzi wa bodi ya hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa


Waziri wa afya maendeleo ya jamii ,jinsia wazee na watoto Dkt.Doroth Gwajima ameupongeza uongozi pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa kwa kuendelea kutoa huduma bora na za kibingwa kwa watanzania wote wanaofika hospitalini hapo .

Pongezi hizo amezitoa wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya wakurugenzi wa hospitali hiyo jijini Dodoma ambapo amewataka kuendelea na moyo wa kusaidia maisha ya watanzania akiamini kuwa kutokana na uongozi bora, imari na wawajibikaji chini ya Dkt.Alphonse Chandika ambae ndiye mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo.

Amesema kuwa hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma bora na hasa zile za kibigwa ambazo tayari wamekwisha Anza na zinakwenda vizuri ,na ametaja huduma za kibigwa na za kwanza kabisa kufanyika katika hospitali hiyo kuwa ni Upandikizaji wa figo na hadi kufikia sasa watu 25 wamekwishakupandikizwa figo.

Pamoja na hayo hospitali ya Benjamini Mkapa inafanya upasuaji wa Moyo na kuziba matundu ndani ya moyo ,Inasafisha figo kwa kuondoa Mawe bila kufanyiwa upasuaji,inafanya upasuaji wa ubongo na mgongo na sasa wameanza huduma ya upandikizwaji wa Uroto kwenye magoti mambo ambayo yalikuwa nadra sana kuyapata katika hospitali nyingi hapa nchini.

Mafanikio haya yamemfanya Dkt.Doroth Gwajima kuagiza uongozi wa hospitali ya Benjamini Mkapa kutumia fursa hiyo kujitangaza ili kusaidia watanzania wengi kujua huduma hizi za kibingwa kuwa zinapatika pia katika hospitali hiyo ili kuwapa unafuu watu waliopo katika ukanda huu jambo ambalo litawafanya kupunguza gharama za safari kwenda kutafuta matibabu hayo katika hospitali zingine ikiwemo hospitali ya taifa Muhimbili (MOI).

Mhe. Doroth Gwajima pia ameipongeza Hospitali hiyo kwa kuwa na utaratibu mzuri wa kupokea maoni kutoka kwa mteja/mgonjwa na kuyashughulikia kwa wakati huku akizitaka hospitali nyingine kuiga mfano huo.


Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt.Alphonse Chandika ambae pia ni katibu wa bodi ya hospitali hispitali hiyo akiwasilisha hotuba yake.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt.Alphonse Chandika ambae pia ni katibu wa bodi ya hospitali hiyo amebainisha kuwa wataendelea kuwatoa huduma bora kwa watanzaina na kwa kudhirisha hilo wameamua kutengeneza mtambo wa kuzalisha gesi ya oksijeni jambo ambalo litarahisisha huduma hiyo kupatikana kwa urahisi akiongeza kuwa mambo huo utakapokamilika na kuanza kufanya kazi itakuwa na uwezo wa kuzalisha mitungi ya gesi mia nne (400) kwa siku jambo ambalo litasaidia kuwa na uwezo wa kusambaza pia gesi hiyo muhimu katika hospitali zilizopo ukanda huo.

Dkt.Chandika amesema kuwa ili kuonesha kuwa mafanikio yanayopatikana ndani ya hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa yatakuwa ni ya ukanda mzima wameamua kununua Gari maalumu kwa ajili ya kusambaza mitungi ya gesi ya oksijeni iliyo na gesi katika hospitali zinazoizunguka ukanda huu wa kati mwa nchi na gari hilo Lina uwezo wa kubeba mitungi zaidi ya 70 kwa mara moja.

Pamoja na hayo Dkt.CHANDIKA amewapongeza wafanyakazi wenzake kwa kuendelea kuchapa kazi kwa uadilifu mkubwa na uaminifu jambo ambalo limeendelea kuifanya hospitali hiyo kupata matokeo chanya kwa jamii ,,akitolea mfano wa maoni yatokayo kwa wateja/Wagonjwa kuwa maoni ya pongezi yameongezeka hadi kufikia 400 swala ambalo limewafanya kuendelea kupata morali ya kazi zaidi.

Dkt.Alphonse Chandika ambae pia ndiye katibu wa Bodi hiyo ameishukuru serikali chini ya Raisi Samia Suluhu Hasan kwa kuendelea kuisaidia hospitali hiyo ikiwemo Nyumba 40 kwa ajili ya wafanyakazi wa hospitali hiyo jambo ambalo litawafanya waendelee kuchapa kazi kwa bidii zote huku wakijua serikali yao ipo nao Bega kwa bega.

Hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa imekuwa na udhubutu mkubwa katika kufanya matibabu ya kibingwa na hii ni kutokana na ushirikiano mzuri walionao na hospitali zilizowatangulia ikiwemo hospitali ya Taifa Muhimbili ,Ocean Road,Bugando ya Mwanza, KCMC ya Kilimanjaro na taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete .

Ni miaka sita sasa tangu kuanzishwa kwa hospitali hii ila inastahili pongezi nyingi kwa kuwa wamejaribu na wameweza kufanya mambo makubwa yaliyoshindikana katika hospitali kongwe hapa nchini na hili limetokana na Uongozi Imara na wafanyakazi waadilifu katika kutoa huduma bora kwa wateja/wagonjwa.

Kwa upande wa Mwanyekiti wa Bodi ya hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt.Deo Mtafiwa ameahidi kuwa bodi itaendelea kuwa bega kwa bega na wafanyakazi wote pamoja na kuwa daraja kati ya hospitali na wananchi ili kuendelea kudumisha huduma bora zinazotolewa na hospitali hiyo kwa ajili ya kufikia malengo waliyojiwekea kwa dhamira njema ya kuhakikisha kuwa huduma zote za matibabu ya kibingwa zitakuwa zinapatikana hapa hapa nchini katika hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa.

MATUKIO MBALI MBALI YA PICHA KATIKA UZINDUZI WA BODI YA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA




No comments:

Post a Comment