TETEMEKO LA ARDHI LAIKUMBA DODOMA, WANANCHI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, January 18, 2022

TETEMEKO LA ARDHI LAIKUMBA DODOMA, WANANCHI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI


Mjiolojia Mwandamizi Gabriel Mbogoni  akizungumza na waandishi wa habari juu ya tetemeko lililotokea usiku wa kuamkia tarehe 18/01/2022 saa saba na dakika ishirini  na nane na sekunde arobaini na nane usiku mkoani Dodoma huku akisema kuwa hakuna madhara yaliyoripotiwa na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari zote pindi inapotokea matetemeko ya Ardhi.

Okuly Julius , DODOMA

TETEMEKO la ardhi lemetokea Mkoani Dodoma ambapo kiini cha tetemeko hilo ni katika safu ya milima ya Chinene iliyopo tarafa ya Haneti wilayani Chamwino.

Akizungumza kuhusiana na tukio hilo,Mjiolojia Mwandamizi Gabriel Mbogoni amesema tetemeko limetokea majira ya saa saba na dakika ishirini  na nane na sekunde arobaini na nane usiku wa kuamkia tarehe 18/01/2022 ambapo hadi sasa hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa baada ya kutokea kwa tetemeko hilo.

MBOGONI ametaja ukubwa wa tetemeko hilo kuwa ni kipimo cha Richter 5 ila ni kubwa kulinganisha na mengine yaliyotokea huku akiongeza kuwa kiwango hicho ni cha kawaida na hakiwezi kusababisha madhara makubwa.

Amewataka wananchi kuwa makini pindi yanapotolea matukio kama haya ikiwemo kutokaa chini ya miti,nyaya za umeme ,Kando ya majengo marefu na kuwataka kutotoka nje au kuingia ndani wakati wa tetemeko ni vyema wakachukua tahadhari kulingana na eneo ulilopo.

Pia amelezea njia mbalimbali za kitaalamu za kupima tetemeko kuwa Kuna skeli mbili zilizotumiwa mara nyingi ni zile za Richter na Mercalli. Katika miaka ya nyuma skeli mpya imeanza kutumiwa kimataifa ni "moment magnitude scale" (kifupi MMS, skeli ya kiasi cha nguvu) inayofanana zaidi na skeli ya Richter lakini iko makini zaidi kwa kutofautisha matetemeko makubwa.


Aidha Mjiolojia huyo amebainisha kuwa teknolojia duniani kote haijaweza kubaini namna ya kutabiri matetemeko ya ardhi huku akiwashauri wananchi kuchuka tahadhari muda wowote hususani katik suala zima la ujenzi kuhakikisha wanajenga nyumba imara kwa kuzingatia taratibu za ujenzi.

Tetemeko la ardhi ni matokeo ya nguvu za asili za mgandamizo ambazo hutoka kwenye matabaka ya miamba katika kina kirefu cha ardhi ambapo wakati mwingine hufika hadi kilomita mia saba kutoka uso wa ardhi ambapo Mkoa wa Dodoma na baadhi ya mikoa ya jirani imekuwa ikikumbwa na matetemeko ya ardhi mara kwa mara kutokana na kuwa kitovu kikubwa cha matetemeko na kwa sababu imepitiwa na bonde la ufa la Afrika Mashariki. 


No comments:

Post a Comment