AWESO:AWAAGIZA WAHANDISI WA MAJI KILA MKOA KUHAKIKISHA WANA MRADI WA KUZINDUA KATIKA WIKI YA MAJI MWAKA HUU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, February 2, 2022

AWESO:AWAAGIZA WAHANDISI WA MAJI KILA MKOA KUHAKIKISHA WANA MRADI WA KUZINDUA KATIKA WIKI YA MAJI MWAKA HUU





Na,Okuly Julius, Dodoma

Waziri wa maji Mheshimiwa Juma Aweso amewaagizi Wahandisi wa Mikoa kuhakikisha wiki ya maji mwaka huu itatumika kuzindua miradi mbalimbali ya maji na kufanya tathmini ya utendaji za idara mbalimbali katika Wizara ya Maji.

Mh.Aweso ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa hafla ya utiaji saini wa hati ya makubaliano kati ya RUWASA na Wizara ya Maji kupitia idara ya Rasilimali za Maji kuhusu utaratibu wa utekelezaji wa miradi ya Mabwawa ya maji kwenye maeneo yanayoratibiwa na RUWASA hapa nchini.


Hata hivyo Mheshimiwa Juma Aweso amebainisha kuwa wiki ya maji mwaka huu itakuwa ni ya tofauti kabisa kwani anatarajia kila mkoa kuwa na mradi wa kuzindua wa maji na amesema kuwa kama kutakuwa na mkoa ambao hawatakuwa na mradi wowote wa kuzindua inabidi Wahandisi wa maji wa mkoa husika wajitathmini.

Pamoja na hayo Mh.Aweso amewapongeza RUWASA pamoja na Idara ya Rasirimali za Maji kwa kuingia makubaliano ya ushirikiano huku akitaka idara zingine kuiga mfano huu kwani itaokoa muda na bajeti kubwa kwa sababu badala ya kila mmoja kufanya kazi kivyake watakuwa wanashirikiana hivyo kazi zitakwenda kwa wakati.

Ameitaka pia Idara ya Rasilimali za Maji mbali na kulinda na kutunza vyanzo vya maji watumie Rasirimali walizonazo kuhakikisha wanaongeza vyanzo vipya vya maji ili kuondoa kabisa adha ya maji nchini

Sanjari na hayo amewataka pia bodi ya mabonde nchini kufanya kazi kwa ubunifu na uweledi mkubwa ili kuhakikisha maji yote yanayopatikana kipindi cha mvua yatumike vizuri na sio kuishia baharini na mengine kuleta maafa.


Amempongeza pia Mheshimiwa Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wizara ya Maji Shilingi bilioni 135 ambazo zitatumika kutengeneza Mabwawa matano, kununu seti za mashine kwa ajili ya kuchimba Mabwawa na kazi nyingine ambayo itakuwa ni faida kubwa kwa watanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali za maji Wizara ya Maji Dkt.George Lugomela amesema kuwa ni historia kubwa kushughudia pande hizi mbili zikitia saini katika hati hii ambapo amebainisha kuwa ujenzi wa Mabwawa matano kwa pamoja ni moja kati ya mambo makubwa kutendeka tangu yeye kuwa mtumishi wa Wizara ya maji takribani miaka ishirini na mbili iliyopita.

Na hivyo kuwataka watendaji katika ngazi za chini nao kuiga mfano huu Kivitendo ili kutatua changamoto za maji katika maeneo yao wanayoyasimamia

Naye Mkurugenzi wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegelo ameipongeza Serikali kwa kugharamia ujenzi wa mabwawa Matano huku akisisitiza ushirikiano kwa watendaji wote ili kupeleka mbele gurudumu la maendeleo katika sekta hii ya maji nchini.



No comments:

Post a Comment