JESHI LA POLISI NCHINI IMETAKIWA KUWEKEZA NGUVU KWA VIJANA KATIKA IDARA YA TEHAMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 21, 2022

JESHI LA POLISI NCHINI IMETAKIWA KUWEKEZA NGUVU KWA VIJANA KATIKA IDARA YA TEHAMA



Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (Katikati)

Na,Okuly Julius, Dodoma 

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew amelitaka jeshi la Polisi kuwekeza kwa vijana katika eneo la TEHAMA kwa sababu ndio njia pekee ya kupambana na makosa ya kimtandao hapa nchini.

Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua Mafunzo ya Mtandao (cybercrime) kwa Wapelelezi na Askari wa chumba cha mashtaka (CRO) itakayodumu kwa siku tano.

Pamoja na hayo amewataka jeshi la Polisi kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi juu ya matumizi mazuri ya mtandao na kufahamu kuhusu ni makosa gani yatamsababishia kuingia katika kosa la mtandao.

Ameongeza kuwa swala la mawasiliano kwa Majeshi yote nchini ni jambo la kuwekewa uwekezaji mkubwa ili kuwasaidia kujiandaa vizuri katika kudhibiti makosa ya mtandao na uahalifu wa aina hiyo kwa ujumla.

Aidha akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini Deusdedit Nsimeki amesema lengo kubwa la haya mafunzo ni kuwajengea uwezo askari hao ili kutambua aina ya makosa ya Jinai.

Naye Kamishina wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi Cp Shabani Hiki wa Jeshi la Polisi amewataka Askari hao kutumia mafunzo hayo katika kuleta matokeo mazuri kwa jamii na mabadiliko ili kuleta taswira nzuri kwa jeshi la polisi.






No comments:

Post a Comment