Korea Kaskazini yasema ilifyatua kombora kujaribu mfumo wa upelelezi - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 28, 2022

Korea Kaskazini yasema ilifyatua kombora kujaribu mfumo wa upelelezi



Korea Kaskazini imesema jaribio la kombora lililofanywa jana Jumapili lilikuwa ni kwa ajili ya kuthibitisha hatua iliyofikiwa katika uimarishwaji wa mfumo wa upelelezi wa kutumia satelaiti hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la Korea Kaskazini KNCA mapema leo siku moja baada ya kufyatua kombora.

Hata hivyo ripoti ya KNCA haikufafanua zaidi kuhusiana na aina ya roketi iliyotumika kwenye jaribio hilo lakini mamlaka nchini Korea Kusini zilisema huenda likawa ni kombora lililofyatuliwa kutoka kwenye eneo linalokaribiana na uwanja wa ndege wa kiamataifa wa Pyongyang. 

Hii ilikuwa ni mara ya nane kwa Korea Kaskazini kufanya zoezi kama hilo kwa mwaka huu na mara ya kwanza tangu mwezi Januari kwa taifa hilo kufyatua idadi kubwa zaidi ya makombora.

                                              CHANZO:DW KISWAHILI 

No comments:

Post a Comment