Alisema mkakati wa Serikali ni kuhakikisha vijana waliofanya vizuri kwenye masomo ya Sayansi wanapata ufadhili (schoolaship) ya kusoma katika vyuo vikuu na mahiri nje ya nchi ili kupata wataalamu wenye uwezo mkubwa.
"Tunahitaji Wanasayansi tuna jukumu la kusomesha Watanzania masuala ya Sayansi, Teknolojiana tiba.
Amezitaka Taasisi kutenga fedha Ili Wanafunzi bora Kabisa wa sayansi wapate ufadhili.
"Tukitenga fedha kila mwaka Watakuwa wakienda kusoma Nchi nyingi zilizoendelea ziliwekeza katika Sayansi tusidhani tuna uwezo wa kutosha," alisema.
Amesema Nchi inahitaji vijana wa kusoma Sayansi na Teknolojia Ili watumike .
Ameongeza kuwa kuna mkakati wa kukutana na Watanzania wanaofundisha Vyuo vikuu vya nje Ili wafungue milango na kuona ni kwa jinsi gani vijana wa Tanzania watapata ufadhili.
"Watanzania wanaofundisha Vyuo vikuu nje ya Nchi tutakaa nao ,watatufungulia milango Ili kuona namna gani vijana wa Tanzania watapata ufadhili," alisema.
Amegusia kuwa mkakati mwingine ni kuongea na balozi mbalimbali Ili vijana wanaofaulu vizuri masomo ya Sayansi wapate ufadhili ambapo pia Serikali nayo itakuwa na mchango wake katika kufanikisha jambo hilo.
" Taasisi zetu Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT) na na Chuo cha Ufundi cha Arusha wanatoa wabumifu wengi lakini tunawapeleka wapi , ," alisema
Pia amesema wanataka Shule zote ziingie kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Serikali itaanza taratibu kuwekeza kwenye Teknolojia na anaamini jambo hilo litasimama.
Mwenyekiti wa Bodi ya TAEC, Profesa Joseph Msambichaka amesema wataanzisha ufadhili (schoolaship) kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye Teknolojia ya nyuklia.
Pia ameongeza kuwa kuna mkakati wa kuanzisha Kiwanda cha Nyuklia nchini ili kwenda sambamba na uwepo wa wataalam wa kutosha.
"Tunategemea kuanzisha mafunzo katika Sayansi ya nyuklia kwa kutumia wataalam waliopo TAEC," alisema.
Pia alitaka kuangaliwa kwa suala la kuondoa tozo ambazo si za lazima katika mionzi.
Mkurungenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Lazaro Busagala amesema Serikali kupitia TAEC imeweka mikakati ya kusogeza huduma karibu na wananchi sawa na mpango wa watu wa maendeleo kwa Taifa.
Amesema ujenzi huo mpaka kukamilika kwake utagharimu Sh bilioni 3.8 gharama hizo ni pamoja na kuweka mandhari nzuri na uzio.
Jengo hilo litakuwa na Ofisi 27 chumba cha mkutano na maabara tano ikiwemo maabara za kupima sampuli ya vyakula na mazingira, maabara ya upimaji wa Viwango vya mionzi kwa wafanyakazi, maabara ya matengenezo ya vifaa vya nyuklia, maabara ya sampuli mbalimbali za mazingira na maabara za ulinzi na usalama wa nyuklia.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya huduma za jamii Abdallah Chikota amesema kamati itaendelea kushirikiana na TAEC Ili wapate fedha za kutosha za kutekeleza majukumu yake.
TAEC ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 7/2003, Awali ilijulikana kama Tume ya Taifa ya mionzi iliyoanzishwa na sheria ya Bunge namba 5/1983.
Majukumu ya time hiyo ni kudhibiti matumizi ya mionzi Nchini kuhamasisha na kuendeleza matumizi salama ya Teknolojia na nyuklia na kufanya Utafiti na kutoa ushauri na taarifa mbalimbali juu ya Sayansi, Teknolojia na nyuklia.
No comments:
Post a Comment