![]() |
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dr.Adolf B. Rutayuga |
Na Okuly Julius, Dodoma
Hayo yemezungumzwa leo jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET)
Dr.Adolf B. Rutayuga wakati wa kikao (WARSHA) na Wakuu wa Vyuo vya Ufundi au vyuo vya kati hapa nchini.
Amesema kuwa Vyuo hivyo vinatoa mafunzo kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na wanasoma mpaka ngazi ya stashahada (Ordinary Diploma) hivyo akawataka wakuu hao kuhakikisha kuwa wanawadahili wanafunzi kulingana na ufaulu wao kulingana na Progaramu ambayo mwanafunzi anataka kuisoma.
Pamoja na hayo Dr.Adolf amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya Vyuo ambavyo vinawachukuwa wanafunzi ambao hawana sifa hivyo wanawasababishia matatizo kwa sababu wao kama Baraza hawawezi kumtambua mwanafunzi huyo kutokana na kutokuwa na sifa katika Programu husika.
"Kuna baadhi ya Vyuo vinaweza kufanya udahili kwa wanafunzi katika programu ambazo hawajapewa idhini na Baraza,au Chuo hakijasajiliwa,mwanafunzi hajakizi vigezo vya kusoma hiyo programu mimi niwaombe wafuate miongozo ya udahili waliyopewa na Baraza ili wasiwaumize watanzania kwa sababu wanalipa ada "Amebainisha Dr.Adolf
Ameleza kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wanasoma hadi miaka mitatu ila mwisho kabisa anakuwa hatambuliki kulingana na sifa ambayo inatakiwa kuwa nayo hivyo maumivu yanaangukia kwa wale wanaolipa ada.
Amewataka wadau wa elimu kuhakikisha wanafuata miongozo ya udahili ikiwa ni pamoja na kuzingatia ufaulu wa D nne kwa wanafunzi wote wanaojiunga na vyuo hivi vya Kati katika masomo kulingana na Udahili wa mwanafunzi.
Amesema kuwa kuna wanafunzi 2854 ambao Vyuo viliwasilisha majina yao na kugundulika kuwa hawana sifa za kusoma Programu mbalimbali ambapo Baraza kwa umakini mkubwa waliweza kugundua hilo na kusitisha udahili wa wanafunzi hao.
"Kama sio umakini wa Baraza basi wanafunzi hawa wote 2854 wangekuwa wamepotezewa muda wao ila Baraza tupo makini na tunayapitia majina yote moja baada ya jingine kwa mfumo wa kielectroniki ili kujiridhisha kuepusha wanafunzi na wanaolipa ada kuingia katika hasara ya kulipia programu na baadae mwanafunzi kutotambulika" Amesema Dr.Adolf
Pia amewataka wakuu wa Vyuo kuwa wawazi kwa wanafunzi wakati wa udahili ili kuondoa hii changamoto inayojitokeza kwa baadhi ya wanafunzi kumaliza masomo na kujikuta hawatambuliki akiwataka pia wanafunzi kutokuwa wakaidi pale wanaposhauriwa kuchagua programu ambazo wana sifa za kusoma kulingana na Ufaulu wao katika masomo.
Kikao ( WARSHA )ya leo imejumuisha wadau kutoka Kanda mbalimbali ikiwepo Kanda ya Kati,Kanda ya Ziwa na Kanda za nyanda za juu kusini ambao ni Wakuu wa vyuo au wawakilishi , Maaafisa Udahili na Vyuo vikuu vinavyotoa Programu za tuzo za ufundi (NTA'S).
No comments:
Post a Comment