![]() |
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (Maelezo), Bw. Rodney Mbuya akieleza jambo wakati wa kikao hicho. |
![]() |
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wafanyakazi Watafiti, Wanataaluma na Washiriki wake (RAAWU), Bi. Jane Mihanji akieleza jambo katika kikao hicho. |
Amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha wadau wa sekta ya Habari cha mashauriano kuhusu utekelezaji wa sheria za kazi.
Ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kuwatumikia wananchi kwa kuwapa huduma bora ni vyema waajiri wakaboresha hali ya mahusiano kazini Ili kuondoa migogoro.
"Sekta ya habari ni sekta muhimu katika kuchangia uchumi wa nchi na Serikali ina wajibu wa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji pia wajibu wa kuhakikisha wanalinda haki za wafanyakazi,"amesema Profesa Katundu
Profesa Katundu amesema kumekuwa na migogoro inayojitokeza Kati ya mwajiri na mwajiriwa inaweza kumaliza kwa njia ya mashauriano .
"Hapo ndio kuna umuhimu wa mwajiri na mwajiriwa kuboresha mahusiano Ili kupunguza majukumu ya kusikiliza migogoro inayojitokeza," amesema.
Amewaambia waajiri ili kuhakikisha kunakuwepo na maelewano mazuri na Serikali pamoja na waajiriwa wao ni lazima wahakikishe wanatebda haki katika ofisi zao.
Pia aliwataka wawekezaji kwenye vyombo vya habari wanapoona kuna ulazima wa kuajiri wafanyakazi kutoka nje ya Nchi Ili kuongeza nguvu katika majukumu yao wasisite kufanya hivyo kwa kufuata taratibu zinazokubalika kwa mujibu wa sheria na taratibu.
"Wakati mwingine unajiuliza ni nani aliye muhimu? Sisi hatuna upande hapo wakati mwingine Kamishina anachukua muda kufanya maamuzi," ameongeza
Mwakilishi kutoka Wizara ya Habari Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (Maelezo) Rodney Mbuya ameitaka sekta ya habari kutumia Teknolojia kuhakikisha sekta inakuwa vizuri zaidi.
" Hii ni nguvu laini, 'soft power 'tuone tumewekeza na kuajiriwa katika sekta muhimu na ina mchango mkubwa katika sekta," amesema..
Naye Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha wafanyakazi , Watafiti, Wanataaluma na Washiriki wake (RAAWU),Jane Mihanji amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kutengeneza ajira za waandishi wa habari.
Ameongeza kuwa wamiliki wa vyombo vya wahabari wamekuwa wakitumia jina la ,'waandishi wa kujitegemea ' Ili kiminya haki zao.
Awali akitoka taarifa Kwa wandishi wa habari Kamishina wa Kazi, Suzana Mkangwa amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kusimamia utekelezaji wa sheria za kazi bà do kumekuwa na changamoto katika utekelezaji wa sheria hizo.
Amesema baadhi ya sehemu za Kazi zimekuwa hazizingatii Viwango vya kazi za staha ,kitu ambacho ni kinyume na haki za binadamu na kinakiuka misingi ya Utawala bora.
Aidha, baadhi ya waajiri wameendelea kutozingatia matakwa ya sheria za kazi na kutowapatia wafanyakazi mikataba ya ajira,kutowapa haki wafanyakazi kujiunga na Vyama vya wafanyakazi ,kutowasajili na kuwachangia kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Pia kuwaachisha kazi wafanyakazi bila kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria pamoja na madai ya mishahara na stahiki zingine za wafanyakazi.
Hali hii imesababisha kutokea malalamiko mengi ya baadhi ya wafanyakazi na waliokuwa wafanyakazi katika sekta muhimu ya habari.
Ameongeza kuwa kutokana na changamoto hizo, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari waliona ni vyema kuwa na kikao cha mashauriano na wadau katika sekta hiyo.
![]() |
Washiriki wakifuatilia kwa makini mada zinazotolewa na wadau wa sekta ya Habari katika kikao cha mashauriano kuhusu utekelezaji wa sheria za kazi |
![]() |
Washiriki wakifuatilia kwa makini mada zinazotolewa na wadau wa sekta ya Habari katika kikao cha mashauriano kuhusu utekelezaji wa sheria za kazi |
![]() |
Washiriki wakifuatilia kwa makini mada zinazotolewa na wadau wa sekta ya Habari katika kikao cha mashauriano kuhusu utekelezaji wa sheria za kazi |
![]() |
Washiriki wakifuatilia kwa makini mada zinazotolewa na wadau wa sekta ya Habari katika kikao cha mashauriano kuhusu utekelezaji wa sheria za kazi |
No comments:
Post a Comment