Na Okuly Julius Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petrol na Dizeli zitakazo anza kutumika hapo kesho huku kukiwa na ongezeko la asilimia 2.54 kwa bidhaa hizo, Huku Mafuta ya taa yakipungua kwa asilimia 3.82 ikilinganishwa na mwezi uliopita.
Akitangaza mabadiliko hayo Jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhe. Godfrey Chibulunje amesema kuwa mabadiliko hayo yamechangiwa na kubadilika kwa Bei za Mafuta katika soko la Dunia , gharama za usafirishaji na thamani ya shilingi ukilinganisha na Dola za Kimarekani.
Kutokana na athari za Vita inayoendelea kati ya Ukrane na Urusi kuathiri soko la mafuta duniani serikali imeghairisha tozo ya Tsh 100 kwa lita ili kumlinda mwananchi na mtumiaji wa mwisho wa bidhaa hiyo muhimu.
No comments:
Post a Comment