![]() |
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Mpawe Tutuba (kushoto) Na Mratibu Mkazi wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Ndugu Zlatan Milisic (Kulia) wakati wa zoezi la utiaji saini wa Mkataba wa Ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Mataifa kupitia Mashirika yake ya Maendeleo. |
Na Okuly Julius Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Mpawe Tutuba ameishukuru Umoja wa Mataifa kupitia Mashirika yake ya Maendeleo kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali na kupitia misaada yao imewezesha kupunguza kiwango cha Umasikini na kukuza uchumi hapa nchini.
Amezitoa Shukrani hizo wakati akifungua Mkutano wa Kutilia Saini Mkataba wa ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Mataifa kupitia Taasisi zake za maendeleo ,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo ofisi za Hazina jijini Dodoma March 24,2022.
Pia Tutuba amesema kuwa kwa sasa kiwango cha umasikini kimesheku kutoka asilimia 38 hadi 26 huku kiwango cha umri wa kuishi kikiongezeka hadi kufikia miaka 65 kwa sasa hapa nchini.
Ameongeza kuwa Programu hii mpya ya Ushirikiano utaipatia Tanzania Trilion 4.3 fedha ambazo zitatumika katika kuendeleza miradi ya maendeleo pamoja na Ustawi wa wananchi katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment