![]() |
| Waziri wa katiba na sheria Mhe,Dkt. Damas Ndumbaro (kushoto) na Mhe,George Simbachawene ambaye sasa ni Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu (kulia) wakati wa kukabidhiana ofisi |
Na Okuly Julius Dodoma
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Ndumbaro amesema kuwa kuteuliwa kwake kwenye Wizara hiyo atafanya kazi kama waziri na wala sio mwanasheria hivyo wataalam waliopo wanapaswa kushauri pale anapopotoka kama mwanasiasa ili kufanya kazi kwa weledi
"Nimekuja hapa kama Waziri/Mwanasiasa sio kama mwanasheria hivyo nategemea sana kutoka kwenu kama wataalamu hivyo mkiona tunapotoka sehemu mtushauri kabla hatujapotea njia niwaombe mimi sio mwanasheria ni Waziri tu,"Mhe,Dkt.Ndumbaro
Awali akizungumza kabla ya kukabidhi ofisi aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo George Simbachawene ambaye sasa ni Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu amesema kazi kubwa ya wizara hiyo ni kusimamia haki na bila haki haiwezekani kuwa na taifa zuri huku akimshauri Waziri Ndumbaro kufahamu mipaka kwakua na ujuzi na umahili katika kushughulikia mambo mbalimbali .
"Ninakufahamu sana najua hapa ndio umefikishwa penyewe sina mashaka na wewe katika kutumia watanzania kupitia Wizara hii kikubwa ni kujua mipaka yake kwa mapana yake maana bila kujua mipaka ya Wizara hii kuna mambo yatakuwa yanaingiliana,"Mhe,Simbachawene
Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene amesema changamoto zilizopo kwenye wizara ya katiba na sheria ni baadhi ya wadau kugeuza haki kuwa uwanja wa taaluma, mchakato wa haki na maamuzi ambayo yamekuwa yakitolewa na vyombo vya haki kama mahakama kutangaza haki lakini mtu aliye tangaziwa haki kutokufikia haki yake.
Hivyo akamtaka Mh.Ndumbaro kuanzia katika eneo hilo ambalo limekuwa linachangamoto kubwa kwa baadhi ya watu wanashinda kesi mahakamani ila hawazile haki zake baada ya kesi kufungwa mahakamani.
Rais samia suluhu hassan alifanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri ambapo waziri simbachawene amehamishiwa ofisi ya waziri mkuu Bunge, Sera na uratibu na waziri damas ndumbaro akihamia wizara ya kariba na sheria, waziri pindi chana akihamia wizara ya maliasili na utalii.



No comments:
Post a Comment