VIDEO:PROF.BEE AZINDUA MFUMO WA KIDIGITALI WA KUTUNZA TAARIFA BINAFSI ZA MGONJWA WA  (MY PERSONAL HEALTH BANK) - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 4, 2022

VIDEO:PROF.BEE AZINDUA MFUMO WA KIDIGITALI WA KUTUNZA TAARIFA BINAFSI ZA MGONJWA WA  (MY PERSONAL HEALTH BANK)



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof.Faustine Bee




Na Okuly Julius Dodoma

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof.Faustine Bee amezindua Mradi wa Benki ya Afya Yangu ya Kibinafsi (MY PERSONAL HEALTH BANK) yenye lengo la kuwasidia wagonjwa kutunza taarifa zao binafsi na kufuatilia data zao muhimu zaidi za afya ikiwa ni pamoja na matibabu yaliyokamilika na yaliyopangwa, uchunguzi, vipimo, ili kuboresha upatikanaji wa matibabu na kuwarahisishia kazi madaktari.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo jijini Dodoma Prof. Bee amesema kuwa mradi wa Benki Yangu ya Afya ya Kibinafsi (MY PERSONAL HEALTH BANK) ni suluhisho la kidijitali ambalo litasaidia kufuatilia na kutoa muhtasari wa data ya afya ya wagonjwa nchini.

"Ninafahamu kuwa lengo kuu la mradi huu ni kuchangia afya njema kwa kuimarisha ubora wa mashauriano ya matibabu kwa kupitia kuboreshwa kwa ufikiaji wa data kamili na ya kibinafsi ya mgonjwa katika programu ya kidijitali."Amesema Prof.Bee

Prof.Bee amesema Kwa upande wa UDOM, mradi huu umekuja kwa wakati mwafaka kwani Chuo Kikuu kimeanza kutekeleza Mpango Mkakati wake mpya wa miaka mitano (2021-2026), ambao unakusudia kutekeleza matarajio ya sasa ya usimamizi wa kuwezesha Chuo Kikuu cha Dodoma kuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu ishirini (20) bora zaidi barani Afrika ifikapo mwaka 2030 kama ilivyoainishwa katika Mpango Mkakati wa UDOM kusudia kubadilisha mafunzo ya udaktari ili kuboresha ubora na wingi wa matokeo ya utafiti.

" Kuna kila sababu ya kuamini kuwa mradi huu ni kichocheo cha kuboresha hali ya kanda ya Chuo Kikuu chetu. wamefahamishwa kuwa mradi huu kimsingi umeundwa kwa majaribio ya majaribio ya matumizi ya mPHB katika mkoa wa Dodoma na baadaye kuongezwa hadi mikoa na nchi zingine barani Afrika,"Amesema

Kwa upande wake Mratibu mkuu wa Mradi huo Dkt.Stephen Kibusi amesema kuwa mradi huo utasidia madaktari kufanya kazi kwa haraka kwani mgonjwa atakuwa na taarifa zake zote hivyo kazi kubwa ya daktari ni kupitia taarifa hizo na kutoa matibabu baada ya kujua histori ya mgonjwa.

Ameongeza kuwa Mradi huo utaanza kutekelezwa katika hospitali sita mkoani Dodoma ikiwemo Hospitali za Wilaya ya Kongwa,Baha na Kondoa pamoja na Hospitali ya Makole ,Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa (BMH).

Katika Zoezi hilo kila hospitali itakuwa na Madaktari wanne ambapo kila Daktari atatakiwa kuhudumia wagonjwa watano kwa siku hivyo baada ya muda mfupi itaonekana faida ya Mradi huo kwa Watanzania.

Mradi huo umefadhiliwa na Chuo Kikuu cha Southern Denmark na MPHB Co.Ltd,kwa kushirikina na Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na MUHAS na utawezesha taarifa za mgonjwa kuongezwa kwenye mfumo na mtoa huduma ya afya na Mgonjwa ataweka taarifa zake za mawasiliano, umri. na data nyingine za msingi.



No comments:

Post a Comment