VIDEO:SERIKALI KUTUMIA BILIONI 49.4 KUAJIRI NA KUWAPANDISHA MADARAJA WATUMISHI 125,223 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 12, 2022

VIDEO:SERIKALI KUTUMIA BILIONI 49.4 KUAJIRI NA KUWAPANDISHA MADARAJA WATUMISHI 125,223

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema, Serikali ya Awamu ya Sita itatumia kiasi cha shilingi bilioni 49.4 kwa mwezi kuajiri na kuwapandisha madaraja jumla ya Watumishi wa Umma 125,223 kabla ya mwaka wa fedha 2021/2022 kuisha ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Jenista amesema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuelezea utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusiana na ajira mpya na usimamizi wa stahiki za Watumishi wa Umma. 

Mhe. Jenista ameainisha mgawanyo wa fedha hizo zitakazotumika kuwa, shilingi bilioni 26,297,541,175.00 zitatumika kuajiri watumishi wapya 32,604 na shilingi bilioni 23,078,224,169.50 zitatumika kuwapandisha madaraja watumishi 92,619. 

Mhe. Jenista amechanganua ajira hizo kwa mujibu wa vipaumbele vya kisekta ambapo Sekta ya Elimu imetengewa nafasi za ajira 12,035, Sekta ya Afya imekasimiwa nafasi za ajira 10,285, Kilimo nafasi 814, Mifugo nafasi 700, Uvuvi nafasi 204, Maji nafasi 261 na Sheria nafasi 513. Waziri Jenista ameeleza kuwa mchakato wa ajira hizo utasimamiwa na Wizara husika, pamoja na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Ameongeza kuwa, licha ya kuajiri na kuwapandisha madaraja watumishi hao, Serikali pia itatumia jumla ya kiasi cha shilingi milioni 824,441,522.00 kuwabadilisha vyeo/kada watumishi 6,026 waliotengewa Ikama na Bajeti ya Mishahara kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 kuanzia tarehe 01 Mei, 2022. 

“Maamuzi haya ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwapandisha vyeo na kuwabadilisha kada Watumishi wa Umma bila shaka yataongeza ari, motisha na uwajibikaji wa hiari kwa watumishi wa umma katika kutoa huduma bora kwa wananchi,’’ Mhe. Amesisitiza.

Amesema, ni wakati muafaka kwa Watumishi wa Umma kuenzi juhudi za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha masilahi ya Watumishi wa Umma kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na bila kushurutishwa 


No comments:

Post a Comment