BRELA YAWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 12, 2022

BRELA YAWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA





Na Okuly Julius Dodoma

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kurasimisha biashara zao ili kukuza wigo wa shughuli wanazozifanya.

Wito huo umetolewa na Afisa Usajili wa BRELA kutoka Kanda ya Kati Bw.Gabriel Girangay wakati wa Mkutano wa Wakandarasi unaofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
"Ili kuendelea kiuchumi na kufungua wigo wa biashara urasimishaji wa biashara ni jambo la msingi,"amesisitiza Bw. Girangay.

Bw.Girangay amewahimiza wadau kuingia wao wenyewe kwenye mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao( online Registration System-ORS) uliopo kwenye tovuti ya BRELA na endapo watahitaji usaidizi wawasiliane moja kwa moja na BRELA badala ya kuwatumia "vishoka" ambao mara nyingi huwapotosha na kusababisha malalamiko.

Aidha ameongeza kuwa kuna faida nyingi kwa wadau kurasimisha biashara zao kwani biashara inaaminika kwa wateja pamoja na taasisi mbalimbali ikiwemo Serikali yenyewe.

Amezitaja huduma zinazotolewa na BRELA kuwa ni pamoja na usajili wa Majina ya Biashara, Usajili wa Makampuni, Usajili wa Alama za Biashara na Huduma, utoaji wa Leseni za Biashara kundi A na Leseni za Viwanda, utoaji wa Hataza sanjali na huduma baada ya usajili.

Mkutano wa Wakandarasi unaofanyika tarehe 12-13 Mei,2022 jijini hapa umebeba kauli mbiu ya “Umuhimu na mchango wa Wakandarasi katka uchumi wa Tanzania,”.

No comments:

Post a Comment