Sambamba na hilo imetaja mkakati wa muda mrefu wa kuchukua mkopo wa gharama nafuu kutoka Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF).
Hayo yameelezwa leo bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Nishati Januari Makamba wakati akiwasilisha kauli ya serikali kuhusu kupanda kwa bei za mafuta na hatua zinazochukuliwa kushughulikia suala hilo.
Akizungumzia kuhusu mkakati wa muda mrefu Waziri Makamba amesema mchakato wa kuchukua mkopo huo upo mbioni kukamilika.
Waziri Makamba ametaja hatua nyingine zisizo za kisekta zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na hali hiyo ikiwemo kuruhusu watu wenye uwezo wa kuleta mafuta kwa bei nafuu kufanya hivyo na kuanzisha Mfuko wa Kuhimili Ukali wa Bei za mafuta.
Mwaka 2020 Dunia ilikumbwa na ugonjwa wa Corona ambapo ili kupunguza makali ya ongezeko la bei ya mafuta nchini,Mwezi Octoba mwaka 2021 ilichukua hatua ikiwemo ya kupunguza tozo katika maeneo mbalimbali.
Uletwaji wa kauli ya serikali bungeni ni utekelezaji wa agizo alilolitoa Spika wa bunge Dokta Tulia Ackson Mei 5 mwaka huu baada ya mbunge wa Kilindi Omary Kigua kutoa hoja ya kuahirishwa kwa bunge ili wajadili suala la upandaji wa bei ya mafuta nchini hoja iliyoungwa mkono na wabunge wote na hivyo bunge kupata nafasi ya kujadili.
No comments:
Post a Comment