Wafanyabiashara wa mbolea wazidi kunolewa - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, May 10, 2022

Wafanyabiashara wa mbolea wazidi kunolewa



Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Kanda ya Nyanda za Juu Kusini - Mbeya leo tarehe 10 Mei, 2022 imefanya mafunzo kwa wafanyabiashara wa mbolea 27 na kuwatunukia vyeti.

Mada zizofundishwa ni pamoja na Sheria ya Mbolea na kanuni zake
Mfumo wa Fis unaotumika mfanyabiashara kujisajili na kusajili mbolea mpya, Aina mbalimbali za Mbolea, matumizi sahihi ya Mbolea na pH ya Udongo,

Virutubisho vya mimea na rutuba ya udongo, Sifa za ghala, kanuni na taratibu za utunzaji wa Mbolea, Matokeo ya Mbolea kwenye mazingira na Utunzaji wa kumbukumbu na wajibu wa mfanyabiashara wa Mbolea. 

Mafunzo haya ni moja kati ya jukumu la mamlaka katika kuwajengea uwezo wadau wa mbolea ili kuwapa uelewa na miongozo inayosimamia tasnia ya mbolea ili wajihusishe na biashara ya mbolea kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment