PROF.MKENDA-MSIISHIE KUJAZA RIPOTI TU TATUENI NA CHANGAMOTO ZILIZOPO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 8, 2022

PROF.MKENDA-MSIISHIE KUJAZA RIPOTI TU TATUENI NA CHANGAMOTO ZILIZOPO


Waziri wa elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akizungumza leo tarehe 9 Juni 2022 wakati wa kikao kazi cha wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya iliyofanyika katika ukumbi wa vijana Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji Prof James Mdoe akizungumza leo tarehe 9 Juni 2022 wakati wa kikao kazi cha wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya iliyofanyika katika ukumbi wa vijana Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wathibiti wakuu wa ubora wa shule wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya iliyofanyika katika ukumbi wa vijana Jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri wa elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amewataka Wathibiti wakuu wa ubora wa shule kutoishia kujaza ripoti badala yake wafuatilie changamoto zinazoikabili sekta ya elimu katika maeneo yao na kutafuta ufumbuzi ili kuendelea kuboresha ukuaji wa Elimu hapa nchini.

Prof.Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 9 Juni 2022 wakati wa kikao kazi cha Tathmini ya utendaji kazi idara ya uthibiti ubora wa shule kati ya viongozi wakuu wa uthibiti ubora wa shule na makao makuu, ithibati ya shule na wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya iliyofanyika katika ukumbi wa vijana Jijini Dodoma.

"Serikali imekusudia kuimarisha ubora wa elimu nchini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa inaakisi mahitaji ya watanzania na utandawazi na kasi ya mabadiliko ya teknolojia kwani soko la ajira limezidi kuwa pana hivyo mabadiliko yanahitajika na ili kufikia malengo hayo ni lazima Wathibiti ubora wa shule wafanye kazi kwa kujituma hasa katika kuhakikisha wanasimamia Miondombinu bora ya kujifunzia"Amesema Prof.Mkenda

Pia amewataka kuhakikisha wanafuatilia wastani mzuri wa walimu kulingana na wanafunzi waliopo katika shule husika kwani kumekuwa na shule nyingi zenye mrundikano mkubwa wa walimu wakati shule zingine zina uwaiano mdogo wa walimu na wanafunzi na kufanya hata ufaulu kwa baadhi ya shule kuwa wa chini kwani mwalimu mmoja unakuta anafundisha wanafunzi wengi kupita kawaida.

"Nendeni mkashughulikie swala la baadhi ya shule kuwa na mlundikano wa walimu wakati kuna shule zingine zina uhaba wa walimu hii nchi ni moja hakuna haki ya mtoto anayesoma mjini wala kijijini wanafunzi wote ni sawa hivyo haki itendeke mimi sioni sababu ya kulundika walimu wengi katika shule moja hapana haki itendeke." Amesisitiza Prof.Mkenda

Pamoja na hayo Prof.Mkenda amesisitiza umuhimu wa malezi kwenye shule kwani watoto wanaanza shule mapema huku wazazi wakiwa kwenye kinyang'anyiro cha maisha hivyo watoto wanakuwa katika mazingira ambayo hayaakisi ufanisi na nidhamu bora kwa mtoto.

"Tunaona kwenye mitandao mambo ya hovyo yanatokea na sisi tusingependa kupuuza tutakuja na tamko na mikakati baada ya kupitia" Amesema Prof.Mkenda na kuongeza kuwa

"Nyie ni mboni ya elimu hapa nchini, mnapaswa kutunzwa, kuheshimiwa na kulindwa ili elimu iweze kuwa bora, hivyo pambaneni serikali imewanunuliwa magari 85 na mambo mengine chungu nzima yanakuja, msichoke"

Waziri Mkenda amesema kuwa Uboreshaji wa elimu kwa kupitia sera ya elimu ya mwaka 2014 na mapitio ya mitaala sio ajenda ya mtu, hiyo ni agenda ya serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo maagizo hayo aliyatoa wakati akihutubia Bunge la 12 tarehe 22 Aprili 2021 Jijini Dodoma.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji Prof James Mdoe amempongeza Waziri Mkenda kwa kuwathamini wathibiti ubora kwa kutenga muda kuhudhuria katika mkutano huo kwani amewaongezea nguvu na ufanisi wa kazi.

Amesema kuwa bila elimu msingi iliyo bora ngazi zingine zote zitakuwa ngumu katika kuthibiti ubora ipasavyo hivyo amewasihi kuongeza weledi kwa ajili ya kazi hiyo.

"Kuna zoezi muhimu sana linaendelea la kupitia mitaala na sera ya elimu na mafunzo hivyo wathibiti ubora wanapaswa kushiriki kwa kina katika zoezi hilo kw kiwango kikubwa kwani haitakuwa na maana kama msiposhiriki" Amekaririwa Prof Mdoe

Kwa upande wake Mkurugenzi wa uthibiti ubora wa shule kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mwl.Euphrasia Buchume amesema kuwa lengo kuu la kuwepo kwa idara ya uthibiti ubora wa shule ni kuhakikisha utoaji wa elimu katika ngazi ya awali,msingi,sekondari,wenye mahitaji maalum na watu wazima inafuata Sera,sheria ,kanuni ,Nyaraka na miongozo iliyopitishwa na wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

No comments:

Post a Comment