TATIZO SIO UBUNIFU BALI NI NAMNA YA KUUFIKISHA KWA WANANCHI-MSUMBA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 9, 2022

TATIZO SIO UBUNIFU BALI NI NAMNA YA KUUFIKISHA KWA WANANCHI-MSUMBA

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Tanzu ya DIT John Msumba Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Taasisi hiyo ya teknolojia ya Dar-es-salaam (DIT) lililopo katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma yanapofanyika Maonesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) 2022
Picha ya pamoja ya baadhi ya wageni na wafanyakazi wa Taasisi hiyo ya teknolojia ya Dar-es-salaam (DIT) katika banda lao lililopo katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma yanapofanyika Maonesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) 2022

Na Okuly Julius-Dodoma 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Tanzu ya DIT John Msumba amesema kuwa taasisi nyingi hapa nchini zina bunifu nyingi ila changamoto inayowakumba ni jinsi gani ya kupeleke bunifu zao kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi .

Hivyo wao kama DIT wameamua kuanzisha kampuni tanzu itakayokuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha bunifu zote zinazobuniwa zinawafikia wananchi na wanazitumia.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Taasisi hiyo ya teknolojia ya Dar-es-salaam (DIT) lililopo katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma yanapofanyika Maonesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) 2022, Mkurugenzi huyo amesema kuwa mbali na kutangaza bunifu hizo pia wanawaendeleza wabunifu hao na kuwajengea uwezo ili waendelee kuzalisha zaidi na kuendeleza bunifu zao.

"Hii kampuni tanzu ya DIT kiukweli inasaidia sana katika kuendeleza bunifu hizi zinazotokana na wabunifu wetu wakiwemo walimu ,wanafunzi wetu na naamini yote haya ni kwa ajili ya kutoa suluhu kwa changamoto inayoikabili jamii"Amesema Msumba

Aidha amesema kuwa Taasisi hiyo kupitia kampuni hiyo Tanzu imegundua mfumo wa kutumia gesi kwenye magari badala ya mafuta na wapo mbioni kuongeza vituo kwa ajili ya kujaza mitungi ya gesi ili ubunifu huo uweze kuwasaidia watu wengi hasa kipindi hiki ambacho kumekuwa na bei kubwa kwa upande wa mafuta.

"Tumebuni mfumo wa kutumia gesi kwenye magari badala ya Petroli hili ni jambo kubwa sana na tutahakikisha huduma hii itawafikia watanzania wote na ili tuwafikie ni lazima tuweke vituo kwenye mikoa mbalimbali na Tayai mchakato umeanza na naamini wananchi wataipokea bunifu hii na kuitumia" Ameongeza Msumba

Pamoja na hayo Msumba ameishukuru ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma kwa kukubali ombi lao la kwenda kufanya maonesho maalumu tarehe 14,juni 2022.

Amemaliza kwa kuwakaribisha wananchi wote kutembele Banda la Taasisi ya Teknolojia Dar-es-salaam (DIT) iliyopo katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ili kujionea bunifu mbalimbali zilizopo pamoja na kuchukua fomu kwa ajili ya kujiunga na masomo kwa watakaohitaji kusoma katika taasisi hiyo na huduma nyingine kulingana na mahitaji ya mwananchi.

No comments:

Post a Comment